logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watoto 2 walioiba iPhone 14 na kuiuza kwa Ksh 8k watwangwa mijeledi waki’dance barabarani

Kichapo kilionekana kuwa kama kichocheo cha densi yao huku wapiti njia wakiwarekodi kwa mbwembwe na madoido.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Dakia-udaku16 November 2024 - 12:32

Muhtasari


  • Kisha waliipiga mnada kwa takribani shilingi elfu 8 tu pesa za Kenya, kwa kutojua thamani yake halisi, jambo ambalo liliwakasirisha watu.
  • Baada ya kukamatwa na kukiri kuiba na kuuza simu hiyo, maskini vijana wa watu walishushiwa kichapo kikali huku wakitakiwa kucheza densi.



Kisa cgha kuskitisha ambacho kimevutia hisia mseto mtandaoni kimeonyesha watoto wawili wavulana wakiadhibiwa vikali barabarani huku wakicheza densi.

Katika klipu hiyo fupi iliyochapiwa kwenye ukurasa mmoja wa TikTok, wavulana hao walionekana wakishushiwa kichapo huku wakicheza densi katika kile kilichoonekana kama ni kushurutishwa.

Inaarifiwa kwamba vijana hao waliiba simu aina ya iPhone 14 pro-max yenye tamani ya zaidi ya laki mbili pesa za Kenya.

Kisha waliipiga mnada kwa takribani shilingi elfu 8 tu pesa za Kenya, kwa kutojua thamani yake halisi, jambo ambalo liliwakasirisha watu.

Baada ya kukamatwa na kukiri kuiba na kuuza simu hiyo, maskini vijana wa watu walishushiwa kichapo kikali huku wakitakiwa kucheza densi.

Kichapo kilionekana kuwa kama kichocheo cha densi yao huku wapiti njia wakiwarekodi kwa mbwembwe na madoido.

Video hiyo ilizua maoni baadhi wakiwahurumia vijana hao na wengine wakiunga mkono adhjabu hiyo kwa kauli kwamba ni vizuri kumkunja kambare angali mbichi.


 


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved