Siku ya Jumanne, Novemba 19, dunia iliadhimisha siku maalum iliyokusudiwa kusherehekea wanaume.
Watu wengi walitumia siku hiyo kusherehekea wanaume muhimu katika maisha yao kwa njia zao za kipekee. Baadhi waliwasherehekea wanaume hao faraghani huku wengine wakichagua kuwasherehekea hadharani.
Mke wa Guardian Angel Esther Musila hakuachwa nyuma, alitumia siku hiyo kusherehekea mwimbaji huyo wa nyimbo za injili pamoja na wanawe wawili Jamal Naibei na Kim.
"Kheri ya Siku ya Wanaume Duniani pacha wangu @_jama1" Bi Musila aliandika chini ya picha ya Jamal.
Pia alichapisha picha nyingine ya Guardian Angel akiwa na Kim, ambao aliwataja kuwa Gs wake.
"Heri ya Siku ya Kimataifa ya Wanaume G's wangu," aliandika.
Bi Musila, ambaye aliolewa na mwimbaji Guardian Angel rasmi Januari 2022, ni mama wa watoto watatu ambao ni Glenn, Kim, na Gilda Naibei. Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 54 hata hivyo hana mtoto yeyote na Guardian Angel.
Katika mahojiano ya mapema mwaka huu, Guardian Angel alisema kwamba anahusiana vyema sana na watoto wote wa mke wake.
“Wao ni watu wakubwa. Tuko na uhusiano mzuri, uhusiano mzuri sana,” Guardian Angel alisema.
Kwa upande wake, Bi Esther Musila alifichua kwamba watoto wake waliingiana vyema sana na mumewe huyo wa miaka 35 tangu mwanzo
Aidha, alifichua kuwa alipoanza kuchumbiana na mwimbaji huyo wa nyimbo za injili, watoto wake walibaini kwa urahisi kwani kulikuwa na mabadiliko makubwa katika tabia zake.
“Siku moja niliwaambia nachumbiana na mtu huyu. Unajua watoto
tu, mimi nikiwa mzazi wao pekee, kulikuwa na dhana kwamba mama amepata mtu,
tutaachwaje peke yetu? Lakini Guardian alikuja maishani mwao kwa kishindo.
Tangu siku ya kwanza nilipomtambulisha kwao, walikuwa na maelewano mazuri,”
alisema.
Huku akiwajibu wakosoaji wa mahusiano yao, Guardian Angel alisema kuwa hajutii kamwe kuchumbiana na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 53.
Alibainisha kuwa wapo wanaume wengi waliooa wanawake wenye umri mdogo kuliko wao, kama ilivyo kawaida katika jamii, lakini ndoa zikashindwa kudumu.
“Ahadi yangu kwa mke wangu inapita zaidi ya umri. Inaenda
zaidi ya maoni ya watu kwa sababu ukiingia kwa hicho kitanda ni wewe na mke
wako, hamna jamaa wa maoni. Kwa kuongea na kuongea mitandaoni,” alisema.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema kwamba tangu mwanzo, hakuwahi kujali watu wangesema nini kuhusu uhusiano wake na mama huyo wa watoto watatu wakubwa.