logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mrembo ‘sidechic’ ajificha ndani ya boot ya gari la mwanamume baada ya mke halali kuwasili ghafla!

Mrembo huyo ambaye alikiri kuwa mpango wa kando kwa mwanamume huyo, alisimulia kwamba walikuwa ndani ya gari la mwanamume huyo wakienda kujivinjari.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Dakia-udaku20 November 2024 - 16:35

Muhtasari


  • Chapisho hilo lilizua maoni kinzani kutoka kwa watu, wengine wakimpongeza kwa kutumia akili na busara kujinasua.



MREMBO mmoja mwenye umri wa makamo amezua mjadala na vichekesho kwenye mtandao wa kijamii baada ya kusimulia jinsi alitumia ujanja wake wa kuzaliwa kukwepa mfarakano na mke halali wa mpenzi wake.

Mrembo huyo ambaye alikiri kuwa mpango wa kando kwa mwanamume huyo, alisimulia kwamba walikuwa ndani ya gari la mwanamume huyo wakienda kujivinjari.

Ghafla, mke halali wa mwanamume wake alitokea na ikambidi kujiongeza na kutafuta njia ya kuponyoka garini ili kuepusha vita na mke halali.

Mrembo huyo alijitosa ndani ya buti la gari hilo na kuvumilia joto kali akiwa hana lolote la kufanya.

“Nilienda kwenye date na mwanamume wa mwenyewe, mke wake karibu atufumanie, namshukuru Mungu aliokoa maisha yangu,” aliandika kwenye video hiyo huku akionyesha jinsi alivyojifinyilia ndani ya buti la gari hilo dogo.

Chapisho hilo lilizua maoni kinzani kutoka kwa watu, wengine wakimpongeza kwa kutumia akili na busara kujinasua.

Hata hivyo, wengine walimsuta kwa kumshukuru Mungu kumuokoa hali ya kuwa alikuwa anafanya jambo lisilofurahisha machoni pa Mungu, tena akiwa anajua.

Hata hivyo, wengine walimsuta wakidai kwamba alisimulia kisa kisichokuwa cha kweli kwa ajili ya kutafuta kiki mitandaoni.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

callmegrace😍🦋: "Nah Mungu akuokoe dada yangu 😂."

Smith: "na wakati huo mke anataka kutumia gari 😂😂😂."

she_is_luchy💖: "nawaooo ooo natamani wanaume wote waliooa waogope kuwa na wake kama hawa."

Selena: "Ninyi watu mnastarehe vipi kuchapisha vitu hivi."



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved