Msani wa muziki wa kizazi kipya Ian Oure maarufu kama Iyanii amekiri kuwa hajawai kushiriki kitendo cha ngono maishani mwake. Iyani alisema hayo katika mahojiano kwenye podikasti moja ya humu nchini.
Mwimbaji huyo wa kibao cha Kifo cha mende, alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo ili kungoja wakati ambao atakuwa kwenye ndoa.
Akiwa kwenye podikasti hiyo, Iyanii alisimulia kuwa muziki wake hutokana na matukio na hadithi ambazo huwa anapiga na marafiki zake.
“Kitu cha kuchekesha kuhusu nyimbo zangu ni kuwa mara nyingi ni hadithi ambazo huwa anapiga.” Alisema Iyanii.
Hta hivyo msanii huyo alisema kuwa anafahamu watu wengi watakosa kuamini maneno yake ila huo ndio ulikuwa ukweli wa maneno.
“Kwa uhakika tangu nizaliwe sijawai shiriki tendo la ndoa tangu nizaliwe, huwa nafikiria kuhusu kuamini kutofanya tendo hilo hadi kwenye ndoa.” Alisema Iyanii.
Kukiri kutoshiriki ngono kwa Iyanii kunajiri licha ya kuimba
nyimbo zenye maudhui hayo. Msanii huyo ameimba nyimbo kama vile Cheat
On Me, Mapenzi na Kifo cha mende ambazo ni ‘kinaya’ na
kauli yake aliyotoa.