Seneta wa Kakamega Boni Khalwale na gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru wameelezea furaha yao baada ya klabu wanayoshabikia katika ligi kuu nchini Uingereza Manchester United, kuanza kurekodi matokeo mazuri tangu kuingia kwa kocha mpya Ruben Amorim mnamo Novemba 11.
Kupitia kurasa zao kwenye mtandao wa X, wawili hao hawakuficha furaha yao baada ya mechi ya Jumapili ambapo Man United iliinyorosha timu ya Everton mabao manne kwa kavu ugani Old Trafford.
Ikiwa ni mechi ya tatu kwa Amorim kuiongoza Man United, timu hiyo imeonekana kuimarika kwani mechi ya kwanza ya Man United dhidi ya Ipswich Town kwenye ligi kuu Uingereza iliishia kwa sare kisha Man United kushinda Bodo/Glimt kwa mabao 3 kwa 2 katika ligi ya Europa Champions League.
Kwa upansde wa seneta Khalwale, alisifia timu ya Man United akisema kuwa hatimaye klabu hiyo ilipata kocha mzuri.
“Khwanyola kochi. Tumepata coach. Ruben Amorim!” Alisema seneta Boni Khalwale.
Kwa upande wake gavana Waiguru, alisifia mchezo wa Man United dhidi ya Everton akiutaja kuwa mchezo bora kutoka kwa klabu hiyo ambayo wachezaji wa Man United hawakuwa na huruma kwa Everton.
“Mabao manne, hakuna huruma. Manchester United walionyesha mchezo mzuri dhidi ya Everton. Hii ndi nguvu tunataka msimu huu wote.” Alisema Waiguru kwenye X akiambatanisha na grafiki ya matokeo ya mechi hiyo.
Hata hivyo inasubiriwa kuona ikiwa Ruben Amorim ataendeleza msururu wa matokeo mazuri.
Amorim alichukua mikoba ya kuiongoza Man United akitokea Ureno ambako alikuwa kocha wa timu ya Lisbon CP.
Kwenye ratiba ya mwezi Disemba ya Manchester United kwenye
ligi kuu ya EPL, itakutana na Arsenal mnamo Jumatano Disemba 4, kisha
Notiingham Forest mnamo Disemba 7, alafu imenyane na Man City ugenini Disemba
15. Mnamo tarehe Disemba 19 itasafiri kucheza dhidi ya Tottenham kombe la
carabao, kisha irejee nyumbani mnamo Disemba 22 dhidi ya Bournemouth, Disemba 26
itacheza dhidi ya Wolves na hatimaye kufunga mwaka dhidi ya Newscastlr manmo
Disemba 30.