Msanii wa muziki wa kizazi kipya Otile Brown amesema kuwa watu wengi hudhania kwamba kuwa na pesa nyingi ndio utajiri.
Kulingana na msanii huo wa kibao cha Samantha, amekanusha dhana hiyo akisema kwamba mtu anaweza kuwa na hela nyingi ila hilo halitoshi kumaanisha kuwa ni tajiri akieleza kwamba utajiri muhimu zaidi ni wa kiroho, kiakili na kimwili ambao umehifadhiwa kwenye nafsi.
“Utajiri wa kweli upo kwenye nafsi na inaanzia kwenye akili.” Alisema Otile Brown.
Kwenye simulizi yake, msanii huyo amesema kwamba sababu inayofanya viongozi wengi kuiba pesa nyingi licha ya tayari ni matajiri ni kwa sababu wanajaribu kufidia kiwewe walicokumbwa nacho katika umri mdogo. Kutokana na hilo, Otile Brown amesema kwamba ni vigumu kwa viongozi hao kubadilisha mawazo yao.
OB amekiri kwamba hiyo ndio sababu inakuwa vigumu kwa viongozi kutosheka na pesa walizonazo.
“Ni kwa sababu wanajaribu kufidia kiwewe walichokuwa nacho utotoni, hawajawai kutosheka.” Alisema Otile Brown.
Otile Brown amesema kwamba baadhi ya viongozi ambao miaka imesonga ni maskini wa kiroho ndio sababu wanajigamba kuhusu utajiri walionao. Hta hivyo Otile Brown amewataka kuvutia kwa njia mbadala kwani tayari ishajulikana kwamba wana pesa.
“Si unaona hizo pesa zote na miaka, bado wanajaribu kujigamba na
kutuonyesha wana pesa. Tayari tushajua mna pesa. Mtuvutie kwa utofauti.” Alisema Otile Brown.