Jamaa mmoja ameelezea kisa cha kushangaza kufuatia kifo cha
mkoi wake.
Kupitia chapisho lake kwenye X, Jamaa huyo aliyefahamika kwa
jina Mrs Zanga alisema kwamba mkoi wake wa kike ambaye alikuwa ni mama wa
watoto 4 alifariki baada ya kukataa kuwekewa damu hospitalini.
Alieleza kwamba walimpeleka hospitalini mama huyo wa watoto
4 na madaktari baada ya kumfanyia vipimo, wakashauri kwamba angehitaji usaidizi
wa damu.
Licha ya kuwepo kwa watu kadhaa ambao walijitolea kumsaidia damu,
mwanamke huyo anaripotiwa kukataa kata kata kuwekewa damu, akisema kwamba hatua
hiyo ni kinyume na Imani za kanisa lake.
Baada ya kukataa kuwekewa damu, aliishia kwa kufa na
kuwaacha wanawe 3, wa mwisho akiwa na umri wa miaka 4 tu.
“Binamu yangu alifariki asubuhi ya leo, akiwa ameacha watoto 3. Mdogo
ana miaka 4. Ni nini kilimuua? Alikataa kutiwa damu
mishipani kwa sababu yeye ni Shahidi wa Yehova,’ Mrs Zanga aliandika.
Baada ya ufichuzi huo ambao hajathibitika kama ni wa kweli,
watu kadhaa walifurika kwenye chapisho hilo na kutoa maoni yao.
@Allezamani aliuliza: "Ujinga huu bado unatokea?"
@highchart alisema: "Pole kwa kupoteza kwako. Simuonei
huruma lakini watoto aliowaacha😩 Mungu atawaongoza na
kuwahifadhi, watakuwa sawa ikiwa wajomba na shangazi ni watu wema wa
kuwatunza"
@MrsZanga alijibu: “Hofu yangu ni kwamba ndugu hawazungumzi
hata wao wenyewe. Wote ni mashahidi wa Yehova, lakini wamekuwa katika uovu wao
kwa wao kwa miaka. Hata sielewi sehemu ya Biblia wanayojifunza 🤦🏾♀️”
@beaubobritton alishiriki: "Nilikuwa na kitu kama hicho
wakati nilifanya kazi katika ER kwa zamu ya usiku. Mwanamke alikuwa anatoka
damu kihalisi na nikamwomba mmoja wa marafiki zangu wa kike aingie na
kuzungumza naye, mwanamke kwa mwanamke, na hatimaye akamfanya mgonjwa akubali
kutiwa damu mishipani 3 ambayo iliokoa maisha yake.”
@ShedakpePerson alifichua: "Nakumbuka wakati marehemu
mjomba wa baba yangu alikuwa katika hali hii. Familia ilikataa. Dkt aliwataka
watoe pesa, kwamba ana njia mbadala ya kumtibu. Kabla hakujapambazuka, Dkt
alimpa damu nyingi.”