Staa wa Bongofleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefunguka kuwa ana mpango wa kuzungumzia wazi uhusiano wake uliovunjika hivi majuzi.
Bosi huyo wa Konde Music Worldwide na sosholaiti Poshy Queen walikuwa wakichumbiana kwa miezi kadhaa kabla ya kuachana miezi michache iliyopita.
Akizungumza kupitia Instagram siku ya Jumanne, mwimbaji huyo alidokeza kuwa hatawahi kufichua mpenzi wake tena kufuatia kuvunjika kwa uhusiano wake wa mwisho.
“Siku
moja nitashare na nyinyi kuhusu mahusiano yangu!!! Niko na uhakika ndio atakuwa
mwisho sitomtambulisha mwingine, Amina,” Harmonize alisema.
Mtunzi huyo wa kibao ‘Single Again’ pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia upendo wake mkubwa kwa mtoto wake wa pekee Zuuh Konde na kusema kuwa binti huyo mdogo ameathiri maisha yake kwa njia nzuri.
Harmonize alidokeza kuwa yeye ni mtu mwenye huzuni na akabainisha kuwa binti yake amemsaidia kupata furaha maishani.
“Naonekana mzuri lakini sina furaha. Asante Mungu kwa upendo wa maisha yangu Zuuh Konde. Bila wewe sijuwi maisha yangu yangekuwaje. Nimepata marafiki wazuri,” alisema.
Wasanii hao wawili wa Tanzania wamekuwa wakichumbiana kwa takriban miezi minane sasa.
Habari kuhusu uchumba wao ziliibuka mapema mwaka huu, na kusababisha mijadala mingi na msisimko kwenye mitandao ya kijamii.
Mapema mwaka huu, Konde Boy alidokeza kuwa uhusiano wake mpya hauhusishi kuficha mambo yoyote akifichua kuwa mwanamke anayechumbiana naye huwa na simu yake wakati mwingine.
"Mwanaume mwaminifu ulimwenguni! Mpenzi wangu huenda na simu yangu ya rununu, tayari ana password ya simu yangu. Iwapo utapata jibu lisilo la kawaida, bado nina upendo nanyi nyote,” alisema Harmonize kupitia Instastories yake.
Mwanamuziki huyo alifichua kuwa alitaka kuchumbuina na mpenzi wake kitambo lakini uhusiano wao haukufaulu wakati huo kama walivyokusudia.
Aidha, aliendelea kutangaza kuwa sasa ametulia kwani mwanamke anayetoka naye sasa hivi atakuwa wa kudumu kwake.
“Hapa ndio mwisho wangu. Onyoo, hajawahi kutembea na yeyote ninayemjua. Mheshimu kama msichana wangu. Popote utakapomuona uache drama!” alisema