Msanii wa bingo fleva D Voice amewataka wasanii wengine nchini Tanzania kutotoa nyimbo katika siku ya mwisho ya mwaka kwa kuwa atakuwa anawachilia video ya wimbo alioshirikishwa na msanii mwenzake Zuchu.
Wasanii hao wawili wanaorekodi nyimbo zao chini ya lebo ya Wasafi Classic Baby maarufu kama WCB, walitoa audio ya wimbo wao mpya kwa jina Hujanizidi uliowachiliwa kwa akaunti ya Youtube ya Zuchu.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye anwani yake ya Instagram, msanii huyo ambaye hivi maajuzi alikuwa nchini Kenya pamoja na Diamond Platnumz kwenye harusi moja eneo la Pwani, amewataka wasanii wengine kuwashabikia kwa video ya wimbo huo badala ya kutoa miziki yao.
D Voice amewaonya wasanii ambao huwa wanasubiri mwisho wa mwaka ndio watoe nyimbo zao kuwa watapata hasara za bure ujumbe huo ukionekana kuashiria kuwa wimbo mpya alioshirikishwa na Zuchu ndio utafuatiliwa mno.
“Wale wasanii wasingeli mnaosubiriaga mtoe nyimbo tarehe 31 mwisho wa
mwaka msitoe maana video yetu ya Hujanizidi inatoka. Ni vyema mngetushabikia
kulikoni kuingia hasara za bure.” Alisema D Voice kwenye ujumbe wake.