Raphael Ssemwanga, mtoto wa pili wa sosholaiti wa Uganda Zari Hassan hivi majuzi aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa huku akiendelea kukua na kuwa mwanamume mkubwa.
Mtoto huyo wa Zari na aliyekuwa mume wake marehemu Ivan Ssemwanga alisherehekea kutimiza miaka 17 na watu waliungana naye kuadhimisha siku hiyo maalum.
Zari alitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kumsherehekea kijana huyo kwa kuchapisha picha zake nzuri.
"Happy birthday to the realest @raphael.tlale," Zari aliandika.
Mtu mwingine maalum ambaye alimsherehekea Raphael hadharani ni mume wa sasa wa Zari, Shakib Cham ambaye pia alikuwa na ujumbe mzuri kwa kijana huyo.
"Heri ya siku ya kuzaliwa @raph, natumai kuwa leo ni mwanzo wa mwaka mzuri kwako," Shakib aliandika chini ya picha ya Raph.
Raph ni mtoto wa pili wa Zari na aliyekuwa mume wake, marehemu Ivan Ssemwanga aliyefariki mwaka 2017, miaka michache tu baada ya wawili hao kutengana.
Kwa sasa ameolewa na Shakib Cham ambaye mara nyingi ameonyesha uhusiano wa karibu na watoto wake wote watano licha ya kutokuwa na mtoto pamoja.