Aliyekuwa afisa wa zamani wa gereza moja nchini Uingereza amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na miezi mitatu jela baada ya mahakama kumpata na hatia ya kushiriki ngono na mfungwa katika video iliyosambaa mitandaoni.
Afisa huyo wa zamani wa gereza, alionekana kwenya video akishiriki mapenzi na mfungwa mmoja mnamo mwezi Juni mwaka uliopita wa 2024.
Katika uamuzi wake, mahakama imeeleza kuwa afisa huyo wa zamani amekuwa akifanya mapenzi mara kadhaa ikiwa ni tabia yake ya kujirudia.
Hata idara ya ujasusi ya polisi inaendeleza uchunguzi kuhusu wafungwa wawili waliotambulikwa kwenye kanda ya video iliyosambaa baada ya tukio hilo.
Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 30, kwa mujibu wa shirika la habari la BBC limearififu kuwa alijaribu kutoroka ila maafisa wa polisi walimkamata katika uwanja wa ndege wa Heathrow katika jaribio la kutorokea Uhispania akiwa na baba wake.
Kufuatia kisa hicho kunadaiwa kwamba wafanyakazi wengi wa kike katika gereza alikokuwa anafanya kazi afisa huyo wa zamani wa gereza, kulikuwa na ripoti za ongezeko la visa vya ngono kutoka kwa wafungwa. Hii ni kwa mujibu wa ujumbe kwa njia wa maandishi kwa mahakama kutoka kwa gavana wa jimbo la Wandsworth Andrew Davy.
Gavana huyo alisema wafanyakazi wengi wa kike katika gereza hilo wameripoti ongezeko la wafungwa kuwataka kimwili na sasa inachukuliwa kuwa mchezo wa haki.
Ushahidi uliowasilishwa kortini vile vile ulionyesha kuwa kulikuwa na tukio lingine mbali na lililosambaa la ngono baina ya afisa huyo na mfungwa huyo mmoja. Kanda za video kwenye camera za mwili kutoka kwa sare rasmi ya kazi ya afisa huyo zilionyesha hivyo.
Aidha wakati wa kusikilizwa kwa kesi dhidi yake mnamo mwezi
Julai, afisa huyo alikiri makosa ya utovu wa nidhamu katika ofisi ya umma
mwezi.