Siku chache baada ya mchekeshaji YY kuweka paruwanja kuwa uhusiano wake na Noela umekwisha, mpenzi wake huyo ambaye wamekuwa kwenye mahusiano kwa muda wa chini ya miezi mitatu alitangamana na mashabiki wake kwenye mtandao wa Instagram.
Noela alichapisha ujumbe wa kuwataka mashabiki kumtumia ujumbe wa sirikwa kuuliza maswali ambayo angeyajibu kwenye matukio yake ya Instagram (Insta Stories).
Hatua hii ya Toywa inajiri muda mchache baada ya YY na mama wa mtoto wake ku’follow kila mmoja na baadaye tena kuacha kufuatiliana kwenye ukurasa wa Instagram.
Wafuasi wa YY na Noela awali waliibua maswali ndani ya mwezi Disemba baada ya YY kukosa kum’post Noela katika siku yake ya mazazi ambapo siku chache kabla ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Noela, alichapisha video akisherehekea siku ya mazazi ya mwanawe alipohitimisha miaka mitatu.
Hata hivyo, shabiki mmoja alitaka kufahamu hali ya mahusiano baina ya Noela na YY ikiwa Noela alikuwa na ushauri wowote wa mahusiano. Kwa upande wa Noela, alimjibu kwa maneno matatu akiashiria kuwa anachoona ni watu wanaopenda mahusiano.
“Naona wapenda mapenzi.” Alijibu Noela Toywa.
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa Instagram alitaka kufahamu namna Noela amejitayarisha kupigana na mawimbi ya mtandaoni.
“Hautawai jua jinsi ulivyo na nguvu hadi wakati unakumbwa na mawimbi
mazito.” Alijibu Toywa.