Seneta wa kaunti ya Narok Ledama Olekina ametania siasa ya Kenya kubadilishwa na kuwa mchezo wa ndondi akirejelea mizozano iliyoshuhudiwa katika mazishi ya mama wa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula iliyofanyika wiki jana katika kaunti ya Bungoma.
Kwenye ukurasa wake wa X, seneta huyo wa aliyechaguliwa kwenye tiketi ya chama cha ODM aliashiria kuwa mwelekeo wa siasa humu nchini umegeuka na mbadala wake ni kufungua viwanja vya ndondi ili wanasiasa kumenyana.
“Mahali hii siasa imetufikisha itabidi sasa tufungue boxing rings! Wacha hii wanaume walimane…” Alisema Ledama Olekina kwenye ukurasa wake wa X awali Twitter.
Kwenye ujumbe wake huo, ujumbe wa seneta Olekina umewalenga viongozi wawili ambapo ametaka gavana wa Trans Nzoia George Natembeya na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah kuwa wa kwanza kwenye mechi ya ufunguzi. Olekina amesema kwamba yeye ndie atakuwa mwamuzi katika mchuano wa ndondi baina ya mbunge Ichung’wah na gavana Natembeya.
“Mechi ya kwanza Natembeya dhidi ya Ichungua. Mimi nitakuwa refa.” Alikiri Ledama Olekina.
Kauli ya Olekina inajiri siku chache baada ya gavana George
Natembeya wa Trans Nzoia na mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah kufokeana
hadharini kwa kutupiana cheche za maneno kuhusu mistakabali yao ya visa vya
utekaji nyara wa vijana ambavyo vilishuhudiwa nchini ndani ya mwezi Disemba.
Kwa upande wake, gavana wa Trans Nzoia alimtaka
rais William Ruto kuhakikisha visa vya utekaji nyara wa vijana unasitishwa kote
nchini huku mbunge Kimani alimkashifu kuwa wakati kiongozi huyo(Natembeya)
akiwa mtratibu wa bonfde la ufa, miili ya wakenya kutoka bonde la ufa ilipatikana
kwenye mto Yala licha ya yeye kuwa kwenye idara ya polisi.