Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka
Tanzania Goodluck Godzbert aligonga vichwa vya habari baada ya kuchoma gari
aina ya Mercedes Benz aliyopewa kama zawadi na Pastor Geo Devi mnamo Desemba
2021.
Katika video ambayo imesambaa mtandaoni, mwimbaji huyo anaonekana msituni, ambapo anatangulia kuegesha gari kabla ya kumwaga mafuta ya taa juu yake, kisha kuendelea kuwasha.
Akitetea matendo yake, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alieleza kwa nini alifanya hivyo;
"Nataka ifahamike kuwa chakula nilichokula siku hiyo na zawadi niliyopewa siku hiyo haikumpendeza Mungu. Badiliko hilo halikuwa sawa."
Mwimbaji huyo alielezea kwa undani sababu ya kuchoma gari. Katika chaneli yake ya YouTube.Gozbert Ministries
Sababu hizo zimetolewa kwa kina katika kipindi cha kipekee chenye sehemu mbili ambapo mwimbaji huyo wa kibao ‘Shukurani’ alisema alikuwa akiliendesha gari hilo kwa muda mrefu kabla ya Mungu kumwambia aache kuliendesha.
"Ilikuwa kwa jina langu, ikimaanisha kuwa lilikuwa gari langu kabisa. Ndiyo maana nililibadilisha kutoka rangi ya fedha hadi nyeusi." alishiriki kwa sehemu.
Aliongeza;
“Kuna wakati nilimpa rafiki gari la kwenda kwenye harusi, alipolirudisha, kwa mara ya tatu yalikuja maelekezo kwamba nisiendeshe gari hilo wala kumpa mtu wa kuliendesha,” alilalamika.
Kwenye video hiyo iliyoonyeshwa kwa mara ya
kwanza Jumapili Januari 26, watazamaji walisikitikia hali yake huku wengine
wakiongeza kuwa imekuwa kifungua macho.
Aliendelea kusimulia; "Mungu anapokuagiza kufanya jambo, hana haja ya kukuambia kwa nini."
Mwimbaji huyo alisema hakuwa na chaguo jingine ila kutii.
"Atakalosema Mungu, nitafuata. Gari limechomwa kwa sababu ninamtumikia Mungu mwenye wivu. Siwezi kulelewa na Mungu halafu mtu anaibuka na kusema yeye ndiye aliyeona kukuzwa kwangu."
Mwimbaji huyo alisema alimwambia mchungaji huyo kwamba aliagizwa na Mungu asiendeshe gari hilo tena.
"Baada ya kumwambia hivyo, kulikuwa na msimu wa habari za uwongo zilizoenezwa kuwa nimekufa. Ilifanyika mara tatu," alisema.
Goodluck Gozbert ni mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili, mzaliwa wa Mwanza Tanzania.
Alianza safari yake ya muziki mwaka wa 2004 alipokuwa akiimba kwaya.
Ana vibao kadhaa vilivyotamba na wimbo wake mmoja wa Hauwezi Kushindana alipata sifa kubwa kutoka kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli.