logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Msani TID adai kwamba ashawahi kuwa kwenye mahusiano na Wema Sepetu

"Nilikuwa kwenye Mahusiano ya mapenzi na wema Sepetu japo ilifika mahali akanitamkia kwamba sikutaki," Alisema.

image
na Japheth Nyongesa

Dakia-udaku30 January 2025 - 15:50

Muhtasari


  • Khalid alifichua hili akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari huko nchini mwao.
  • Alidai kwamba maamuzi ya wema Sepetu kumuacha yalikua pigo kwake na yalimuacha na tabia tofauti kabisa.


Mwanamuziki wa Bongo fleva tokea nchini Tanzania Khalid Muhamed maarufu TID amedai kwamba ashawahi kuwa kwenye mahusiano na mwigizaji wa filamu Wema Sepetu.

Baadhi ya kazi nzuri alizowahi kuzifanya msani TID ni pamoja 'Nyota Yako' na 'Siamini.'

TID alifichua haya akiwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari huko nchini mwao.

"Nilikuwa kwenye Mahusiano ya mapenzi na wema Sepetu japo ilifika mahali akanitamkia kwamba sikutaki. Tangu kipindi hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikiwa Wema Sepetu anataka Kurudi hakuna nafasi tena " I' m occupied" alisisitiza mwimbaji huyo wa Bongo.

Kwenye usiku wa RnB uliokuwa umeandaliwa na The Bridge Show ya Mlimani TV, Kulikuwa na wasanii wengi ambao walikuwa na shughuli ya kuperfom.

Msani Khalid aliwashangaza wengi alipodai hadharani mbele ya umati kwamba ashawahi kuwa kwenye mahusiano ya mapenzi na Wema Sepetu mwigizaji wa filamu za bongo.

Matamshi hayo yaliwafanya baadhi ya mashabi kuhisi vibaya na kuanza kumzomea mwanamziki TID akiwa jukwaani. 

TID aliwahi kudai kwamba wakati akiwa kwenye mapenzi na Wema Sepetu ndio muda ambao aliwahi kutengeneza pesa mingi sana kimziki.

Alidai kwamba maamuzi ya wema Sepetu kumuacha yalikua pigo kwake na yalimuacha na tabia tofauti kabisa.

Alisema kwamba kipindi akiwa na Wema Sepetu alindikwa sana kwenye magazeti na mitandao, hakulifurahia sana jambo hilo ila uilimbidii kwa wakati huo. 

Baada ya Khalid kuachwa kimapenzi na Wema Sepeti alikuja kuachia kilio chake kwenye wimbo wake wa 'Nilikataa' akiwashirikisha Mr Blue na Q chief.

Wema Sepetu pia amewahi kuwa kwenye Mapenzi na watu maarufu nchini Tanzania, akiwemo mwanamziki maarufu wa bongo Diamond Platinumz pamoja na aliyekuwa mwingizaji maarufu wa filamu Marehemu Steven Kanumba.




RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved