logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wasiwasi kuhusu uhusiano wa Khalif Kairo na Wavinya Maria

Mienendo ya wawili hao ya hivi maajuzi katika mitandao ya kijamii huande inaashiria kuvunjika kwa safari ya mapenzi.

image
na Japheth Nyongesa

Dakia-udaku30 January 2025 - 03:25

Muhtasari


  • Mambo yanaonekana kubadilika. Ingawa bado wanafuatana kwenye mitandao ya kijamii, hawashiriki tena picha au video pamoja.
  • Zaidi ya hayo, wamefuta picha walizokuwa nazo wakiwa pamoja hapo awali kutoka kwa kurasa zao.


Mienendo ya wawili hao ya hivi maajuzi katika mitandao ya kijamii huanda inaashiria kuvunjika kwa safari ya mapenzi miongoni mwa wawili hao ambayo imekua ikiyumbayumba.

Wavinya Maria ni mwanamitindo na mrembo wa Kenya ambaye alitawazwa kuwa Miss World Kenya 2019. Aliwakilisha Kenya katika Miss World 2019 na aliwekwa katika 12 bora.

Khalifa kairo  awali alikuwa katika uhusiano na mshawishi Cera Imani. Hata hivyo alisonga mbele kwa haraka sana na Wavinya Maria, malkia wa zamani wa urembo.

Uhusiano wao ulitangazwa sana, huku Kairo mara nyingi akimsifu Wavinya kwa kuwa mwanamke mcha Mungu ambaye alimsukuma kuwa mwanamume bora.

Hata hivyo, katika wiki za hivi karibuni, mambo yanaonekana kubadilika. Ingawa bado wanafuatana kwenye mitandao ya kijamii, hawashiriki tena picha au video pamoja kama walivyokua wamezoea.

Zaidi ya hayo, wamefuta picha walizokuwa nazo wakiwa pamoja hapo awali kutoka kwa kurasa zao. Hii imezua uvumi kwamba huenda wametengana.

Akiongezea wasiwasi huo, Wavinya alikuwa ametoweka kwenye mitandao ya kijamii lakini hivi karibuni alirudi. Alichapisha picha na video mpya, akidai kuwa yuko katika "enzi yake tulivu"

Khalifa Kairo ambaye ni mfanyabiashara wa magari kwa sasa anaandamwa na kesi inayomuhusisha na utapeli kwa kilayanti wake ambaye hawakumalizana vizuri.

Inadaiwa kwamba mteja wake alimpa milioni 2.2 kwa ajili ya biashara ya ununuzi wa gari ila jambo ambalo amekiri ila makubaliano yako hayakukamilika.

Kairo ilimbidii kugeukia wahisani kumusaidia baada ya kukamatwa kwa mara ya pili siku chache tu baada ya kuachiliwa kwenye kesi tofauti.

"Baada ya kuhudhuria kutajwa kwa kesi katika mahakama za Milimani, nilikamatwa tena na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Parklands.

Tumejaribu kuhakikisha tunafanikisha makubaliano lakini vyombo vya habari na ushiriki wa polisi mara wanatuweka katika maji ya kina na kuathiri sana uwezo wetu wa kufanya kazi. Ofisi zetu zote zimefungwa kwa sasa.

Nimekuwa na miaka kumi ya kuvutia katika biashara bila kesi ya uhalifu unaohusu magari,  maelfu ya watu wamefanikiwa kununua magari kutoka kwangu.

Kutokana na masuala ya kisheria, kampeni yetu ya wafadhili ilifungwa usiku wa jana.

Yote yatapita hata hivyo, Ninawaomba wafuasi wangu, marafiki, wateja wa zamani na washirika wasaidie kwa kiasi chochote wanachoweza kutupa support ya kupigana dhidi ya vikosi visivyojulikana ambavyo vinahujumu kampuni yangu," aliandika Kairo katika mtandao wake wa X.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved