Mwanamuziki wa bongo nchini Tanzania Diamond Platinumz alisafiri kwenye msafara wa kifahari alipokuwa akielekea Zanzibar kwa ajili ya kufanya show kwenye tuzo za Trace Awards.
Mfanyibiashara mkubwa wa magari nchini humo Issa Tambuu sasa amejitokeza na kusema kwamba msafara huo ulikuwa wenye thamani ya zaidi ya bilioni mbili.
Issa Tambuu alikuwa anazungumza kwenye mahojiano na mwanahabari ambaye alitaka kujua ni vipi alichukulia tukio hilo kama yeye kibinafsi kama mtaalamu wa magari.
"Ile ni kama zaidi ya bilioni mbili, yale magari ni ya gharama sana," alisema mwanabiashara huyo.
Tambuu pia amaempongeza Diamond akisema ni kawaida ya wanamziki kufanya hivyo kutafuta umaarufu maana hilo ndilo linalowaweka na alieleza kwamba alifurahishwa.
"Mimi nimefurahi, kile ni kitu kizuri, tunanunuwa gari ili litusaidie kwenye usafiri na bahati nzuri serikali ya Zanzibar na serikali ya muungano wa jamuhuri ya Tanzania imeeleza vizuri kwamba ukiwa na chombo chako cha moto unaruhusiwa kwenda nacho kule, msingi umefuata sheria iliopo na walioko Zanzibar pia wanaruhusiwa kuvuka nacho," alieleza.
kwa hivyo Simba aliona kule atakuwepo kwa zaidi ya wiki au siku tatu, yeye ni msani mkubwa anaitaji attention, na hiyo attention itahitaji usafiri, yale magari ni ya gharama kuyapakia kwenye meli, sasa labda anghetafuta mengine angeyapata wapi. mimi nimeona ni kitu kizuri na nimependa. pale wanakutana wasani wengi wengi kutoka mataifa mbali mbali na 'status" ya msani inahitajika ionekane. kwa kifupi mwenyeji wa mashindano lazima aoneshe," alienndelea.
Mfanyibiashara huyo pia amesema kwamba msanii yeyote siku zote ni kukuza jina lake na Diamond kufanya hivyo hajakosea.
Alichokifanya ni kuingiza mapato, na msani kama ana uwezo basi anafaa kutumia chochote kukuza "brand" yake," alisema.