logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Pasta Amuua Bintiye, 16, Akidai ‘Ni Mchawi Anayejibadili Kuwa Nyoka’

MWANAMUME mmoja anayefahamika kama mchungaji katika kanisa moja ameripotiwa kumuua bintiye mwenye umri wa miaka 16 anayeigua ugonjwa wa Down Syndrome

image
na MOSES SAGWEjournalist

Dakia-udaku03 March 2025 - 13:14

Muhtasari


  • Baada ya muda mrefu, Pasta aliwaita watoto wake ndani na kutangaza kufariki kwa binti huyo.
  • Aliyeshiriki chapisho hilo aliyetambulika kwa jina la @EduEle5 kupitia ukurasa wa X, alifichua kuwa polisi wamepewa taarifa na mchungaji huyo kwa sasa yuko mbioni.
  • Mamlaka imeanzisha msako na pia inaomba umma usaidizi wa kumpata na kumkamata.

Biblia

MWANAMUME mmoja anayefahamika kama mchungaji katika kanisa moja ameripotiwa kumuua bintiye mwenye umri wa miaka 16 anayeigua ugonjwa wa Down Synbdrome aimtuhumu kama mchawi.

Tukio hili la kushtua lilifichuliwa katika chapisho lililosambaa kwenye jukwaa maarufu la mtandao wa kijamii, X, lililojulikana kama Twitter.

Ndugu mdogo wa msichana huyo alisema baba yao alikusanya familia na kutangaza kifo chake baada ya tukio hilo.

Ndugu mdogo alikumbuka kufungua mlango kumsaidia Dadake kutupa kinyesi chake wakati baba yao alipoingilia kati, akisisitiza ashughulikie mwenyewe. Alitii lakini akaanguka huku akirudi chumbani kwake.

Kijana alisema alimjulisha baba yao, ambaye aliingia chumbani na kuwaambia wengine waondoke wakati yeye akimuhudumia bintiye. Baada ya muda mrefu, Pasta aliwaita watoto wake ndani na kutangaza kufariki kwa binti huyo.

Aliyeshiriki chapisho hilo aliyetambulika kwa jina la @EduEle5 kupitia ukurasa wa X, alifichua kuwa polisi wamepewa taarifa na mchungaji huyo kwa sasa yuko mbioni.

Mamlaka imeanzisha msako na pia inaomba umma usaidizi wa kumpata na kumkamata.

Chapisho hilo lilisomeka, “Mtume Ubong Bassey Etim alimuua bintiye mwenye umri wa miaka 16 huko Calabar baada ya kumshutumu kuwa mchawi ambaye angeweza kubadilika na kuwa nyoka. Msichana huyo mchanga, ambaye alikuwa na ugonjwa wa Down, aliuawa kikatili mnamo Februari 15, 2025, huko Calabar, Jimbo la Cross River.”

“Mke wa mshukiwa aliyeachana naye alifichua kwamba pasta alikuwa na historia ya unyanyasaji wa nyumbani, ambayo ilimlazimu kutoroka nyumbani kwao. Pamoja na hayo, aliendelea kupigania usalama wa watoto wake. Sasa anatoa wito kwa kusaidia kuhakikisha bintiye anapata haki.”

Tazama chapisho hilo hapa;


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved