logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee adokeza kilichomvutia kwa mpenziwe mzungu 'Omondi'

Alijigamba kuwa mahusiano yake mapya yamefanya akawa mwenye furaha zaidi na kuongeza urembo wake.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri11 October 2022 - 06:07

Muhtasari


•Akothee amedokeza kuwa bidii kubwa ya mzungu huyo ambaye amepatia jina Omondi ndiyo iliyomvutia kwake.

•Mama huyo wa watoto watano alidokeza kuwa mpenzi wake mpya ni tajiri mkubwa.

Mwimbaji na mjasiriamali mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee ameendelea kufurahia mahusiano yake mapya na mpenziwe mzungu.

Kwa muda sasa Akothee amekuwa akichumbiana na mwanaume wa makamo aliyetambulisha kama Bw Schweizer baada ya kutengana na Nelly Oaks mapema mwaka huu. Siku za hivi majuzi amekuwa akiomuonyesha mpenziwe mpya mara kwa mara.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 sasa amedokeza kuwa bidii kubwa ya mzungu huyo ambaye amepatia jina Omondi ndiyo iliyomvutia kwake.

"Habari za asubuhi wafalme na malkia. Mnaona sababu kwa nini Bwana Omondi aliuteka moyo wangu. Huwa ameamka kabla ya saa kumi na moja asubuhi, aah Mungu huyu💪💪💪💪.. na ndio maana nilimpatia jina Omondi," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumanne asubuhi.

Aliambatanisha ujumbe huo na picha inayomuonyesha akiwa na mpenzi wake wakitembelea shamba lake. Wawili hao walionekana wakizunguka shamba hilo kubwa na kuzungumza na wafanyakazi waliokuwa pale.

"Ndio mpenzi ni yetu yote, pia tunamiliki mto, bado wewe uweke bwawa la samaki na tuongeze utajiri mara tatu," alimwandikia mpenziwe.

Katika chapisho lake lingine, mama huyo wa watoto watano alidokeza kuwa mpenzi wake mpya ni tajiri mkubwa.

Pia alijigamba kuwa mahusiano yake mapya yamefanya akawa mwenye furaha zaidi na kuongeza urembo wake.

"Lakini huyu mzungu wangu amefanya nimekuwa mrembo na mwenye furaha sana, haki pesa wewe ni sabuni ya mapenzi. Hakuna kitu tamu kama kuchumbiana na mwanaume ako na pesa zake. Tamuuuu," alisema.

Akothee alitangaza mahusiano yake mapya mwezi uliopita baada ya kumficha mpenziwe hadharani kwa muda mrefu.

Haya yalitokea miezi kadhaa baada ya kuvunjika kwa mahusiano yake ya awali na aliyekuwa meneja wake Nelly Oaks.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved