logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Akothee apigwa na butwaa baada ya mumewe mzungu kumtambulisha kama "My Rosecoco"

Akothee alionekana kushangaa kama kwamba mumewe Omosh alijua maana ya jina alilomwita.

image
na Radio Jambo

Habari03 June 2023 - 07:48

Muhtasari


•Bw Omosh, alimminia mahaba mkewe Akothee na kujigamba kumhusu huku wakiendelea kufurahia fungate nchini Ugiriki.

•Omosh alielezea furaha yake baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43.

Siku ya Ijumaa, mume wa Akothee, Denis Shweizer, almaarufu Omosh, alimminia mahaba na kujigamba kumhusu huku wakiendelea kufurahia fungate nchini Ugiriki.

Wapenzi hao waliofunga ndoa mwezi Aprili mwaka huu wamekuwa wakiburudika pamoja katika jiji zuri la Santorini kwa wiki nzima na wote wamekuwa wakionyesha baadhi ya matukio ya kumbukumbu wanazotengeneza pamoja jijini humo.

Katika chapisho lake la hivi punde zaidi, Omosh alionyesha video ya mkewe akitembea kwa furaha katika mitaa ya mji huo wa Pwani.

"My roscoco"  Omosh aliandika kwenye video hiyo aliyochapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Huku akijibu kwenye chapisho hilo, Akothee alionekana kushangaa kama kwamba mumewe mzungu alijua maana ya jina alilomwita.

"Unajua maana ya roscoco weweee?" alihoji.

Mapema siku hiyo, Omosh alielezea furaha yake baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 43.

Alichapisha picha yake nzuri na Akothee wakifurahia muda baharini huku wakionekana wenye bashasha tele.

"Kuwa na kushikilia. Siku yangu ya kuzaliwa na kila kitu changu baharini, ningetaka nini zaidi?" alisema kwa Kijerumani.

Mswidi huyo aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mnamo Mei 31.

Huku akimsherehekea mumewe kwenye Instagram, mwimbaji Akothee alisema ana bahati kuwa mke wake.

"Denis Eduard Schweizer Omondi wa 7 amekuwa mwanaume wa aina yangu. Siku zote nimekuwa nikitaka mtu ambaye anaweza kuchafua mikono yake, mwenye nguvu, kichaa, mwenye upendo, mwenye kuudhi na zaidi ya yote mwenye kujali," Akothee aliandika Jumatano na kuambatanisha na picha za mumewe.

Aliongeza, "Siku zote nimekuwa nikitaka rafiki ndani ya mahusiano, mtu mwenye nia wazi na mwenye kuelewa kwa hali ya juu kwa sababu AKOTHEE ni taasisi yenye matawi mbalimbali ya wazimu. Mwanaume mwenye wazimu kidogo tu ndiye anayeweza kumuelewa Esther, Esther si mwanamke wa wavulana, anavutia wanaume na kuwatisha wavulana, ndio maana AKOTHEE NDIYE KIPIMO CHA MAFANIKIO."

Mama huyo wa watoto watano aliweka wazi kuwa hana majuto yoyote ya kufunga pingu za maisha na mzungu huyo.

“Nilikuchagua wewe na huyo ni mume wangu hapo,” alisema.

Akothee pia alitumia fursa hiyo kumkumbuka ambaye angekuwa mtoto wao wa kwanza pamoja ambaye angezaliwa miezi miwili ijayo.

Licha ya kupoteza ujauzito wake miezi kadhaa iliyopita, alimhakikishia Omosh kuwa watapata mtoto pamoja hivi karibuni.

"Nina furaha sana kuanza safari mpya. Mister Omosh ungeweza kuwa baba tarehe 22 Julai 2023 lakini ya ulimwengu hutokea na tutakuwa wazazi tena hivi karibuni mpenzi wangu. Niruhusu nikutakie kheri njema. Kheri ya siku ya kuzaliwa mfalme wa umalkia wangu. Heri ya siku ya kuzaliwa  Omondi wa saba," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved