Akothee hatimaye aenda hospitalini kupachikwa ujauzito wa mtoto wa sita

Alidokeza kuwa angependa kupata mapacha kwa kuwa ana hamu ya watoto.

Muhtasari

•Ijumaa asubuhi mama huyo wa watoto watano alitangaza kwamba yupo hospitalini tayari kwa shughuli hiyo kufanyika.

•Akothee aliweka wazi kuwa mtoto ambaye atakayemzaa atakuwa na baba lakini atamficha kutoka kwa wanamitandao.

Image: INSTAGRAM// AKOTHEE

Hatimaye shughuli ya upanzi wa mbegu ya kiume kwenye tumbo ya uzazi ya Akothee imeratibiwa kufanyika leo nchini Ufaransa.

Ijumaa asubuhi mama huyo wa watoto watano alitangaza kwamba yupo hospitalini tayari kwa shughuli hiyo kufanyika.

Wakati huo huo Akothee aliweka wazi kuwa mtoto ambaye atakayemzaa atakuwa na baba lakini atamficha kutoka kwa wanamitandao.

"Tupo kwa daktari leo. Na  mtoto wetu ana baba. Ni kwamba hautawahi kumuona kwenye mitandao ya kijamii, hapa kuna uchawi wa mahusiano," Akothee alitangaza kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 42 pia alidokeza kuwa angependa kupata mapacha kwa kuwa ana hamu ya watoto.

Takriban wiki moja iliyopita mwanamuziki huyo alifichua mpango wake wa kupachikwa ujauzito katika hospitali ya Ufaransa.

Alisema alichagua njia ya Artificial Insemination  kwa kuwa hakuna dalili za yeye kupata mwenzi hivi karibuni.

Nina hisia fulani kwa watoto. Ninakosa kitu na sitaki kupata ujauzito nikiwa na miaka 45, na kwa kuwa inaonekana wazi kwamba huenda sitapata mwenza hivi karibuni nimeamua kutafuta mtoto kwa njia ya Artificiial Insemination hapa Ufaransa,”Aliandika kwenye Instagram.

Aliwataka watu kutohoji kuhusu mhusika wa ujauzito wake na kusema anachotaka ni mtoto wake pekee bila drama zozote.

"Fanya unachotaka na maisha yako, ni maisha yako," Alisema.

Ujauzito ambao mwanamuziki huyo atabeba utakuwa wake wa sita.

Akothee tayari ana watoto wengine watano ambao alipata na wanaume watatu tofauti. Wawili kati ya wanaume hao ni wazungu ilhali mmoja ni Mkenya.

Mwanamuziki huyo ana watoto watatu wa kike (Vesha Okello, Rue Baby, Fancy Makadia) na wawili wa kiume (Prince Ojwang' na Prince Oyoo) ambao ndio wadogo.