logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Bega langu kulilia" Kajala amwaga mahaba kwa mwanaume mwingine baada ya kumtema Harmonize

Kajala ameonyesha upendo mkubwa kwa mwanaume aliyemtambulisha kama 'bestie'  wake.

image
na Radio Jambo

Habari10 January 2023 - 07:56

Muhtasari


•Kajala alikuwa akimsherehekea Junior Sniper, kama alivyotambulishwa kwenye Instagram, alipofunguka kuhusu mapenzi aliyonayo kwake.

•Aliendelea kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Muigizaji mkongwe wa filamu Bongo Frida Kajala Masanja ameonyesha upendo mkubwa kwa mwanaume aliyemtambulisha kama 'bestie'  wake.

Kajala alikuwa akimsherehekea Junior Sniper, kama alivyotambulishwa kwenye Instagram, alipofunguka kuhusu mapenzi aliyonayo kwake.

Mpenzi huyo wa zamani wa  staa wa Bongo Harmonize alimkumbusha Sniper kuhusu umuhimu wake mkubwa katika maisha yake.

“Bega langu la kulilia, bestie wangu, fahamu tu kwamba wewe ni muhimu sana kwa mimi na nakupenda mpaka nakupenda tena,” aliandika chini ya video yake akicheza na kusherehekea na rafiki huyo wake wa karibu.

Aliendelea kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa.

Katika video ambayo alichapisha, yeye na rafiki yake huyo walionekana wakinengua viuno na kushiriki wakati mzuri pamoja katika eneo la burudani ambapo muziki wa sauti ya juu ulikuwa ukipigwa.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 kudokeza mpango wa kupata mtoto mwingine.

Katika chapisho la Instagram siku ya Jumapili, mama huyo wa binti mmoja alidai sasa ni wakati mwafaka wa yeye kupata mwingine.

"Nadhani sasa ni muda sahihi wa kupata mdogo wako dada Pau (Paula)," aliandika kwenye Instastori zake.

Ujumbe huo ulionekana kuelekezwa kwa bintiye wa pekee Paula Paul ambaye alimleta duniani takriban miongo miwili iliyopita.

Meneja huyo wa zamani wa Konde Music Worldwide zaidi alifichua kwamba hatatumia tena dawa za kuzuia mimba kuendelea.

"Hakuna kutumia P2 tena, niko tayari kuwa mama tena," alisema.

Kajala hata hivyo kufichua kama tayari yuko kwenye mahusiano mengine baada ya kumtema Harmonize mwishoni mwa mwaka jana.

Ujumbe wake hata hivyo iliibua shaka na dhana kuwa huenda tayari kuna mwanaume mwingine katika maisha yake.

Kajala alitangaza kutengana na Harmonize mwezi Desemba baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miezi minane. Wawili hao walikuwa wamerudiana mwezi Mei baada ya Harmonize kuomba msamaha.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema Desemba 2022  kupitia Instagram.

Aliendelea kufichua kwamba tayari amemsamehe bosi huyo wa Kondegang na kusema yuko tayari kupiga hatua nyingine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved