logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond akejeliwa kwa Kiingereza kibovu baada ya kumwambia Derulo alifika saa ‘2nd in the morning’

Wanamitandao, hasa Wakenya sasa wameendelea kutoa maoni mseto kuhusu Kiingereza cha mwimbaji huyo.

image
na SAMUEL MAINA

Burudani31 July 2024 - 08:05

Muhtasari


  • •Katika video, wawili hao wanasikika wakizungumza kwa lugha ya Kiingereza ambapo Diamond alisikika akitumia kiingereza vibaya kujieleza.
  • •Wanamitandao, hasa Wakenya sasa wameendelea kutoa maoni mseto kuhusu Kiingereza cha mwimbaji huyo.

Staa wa Bongo, Naseeb Abdul Juma almaarufu Diamond Platnumz, anavuma kwa mara nyingine tena na kukejeliwa kwenye mitandao ya kijamii kwa sababu ya Kiingereza kibovu.

Bosi huyo wa lebo ya WCB hivi majuzi alikutana na mwimbaji wa Marekani, Jason Derulo, na kushiriki wakati mzuri pamoja. Walifanya hata colabo ya wimbo wa Diamond, ‘Komasava.’

Video ya mkutano wa wanamuziki hao wawili sasa imeteka hisia za watumiaji wa mtandao. Katika video, wawili hao wanasikika wakizungumza kwa lugha ya Kiingereza ambapo Diamond alisikika akitumia kiingereza vibaya kujieleza.

“Ulifika lini mjini?” Jason Derulo alisikika akimuuliza Diamond.

Diamond alisikika akijibu kwa kiingereza kibovu, “2nd, right? 2nd in the morning.”

Katika video hiyo, msanii mwingine alisikika akimuuliza staa huyo wa bongo fleva kama yeye ni dansa. Alijibu kuwa yeye ni mwanamuziki anayeweza kucheza densi.

Wanamitandao, hasa Wakenya sasa wameendelea kutoa maoni mseto kuhusu Kiingereza cha mwimbaji huyo. Wengine wamemkejeli huku wengine wakiendelea kumtetea; -

Tazama maoni kutoka kwa baadhi ya wanamtandao; -

Vickyndungu: If I had his kind of money, I would even say twoond in the morning.

Maryam_amoo732: We speak English the way white people speak our Swahili period.

Skili_peng: English is not our language. No need for criticism.

African_melanie: as long as he knows how to transfer money, speaking in English is not a problem.

Malika_staudinger: After kusema am 31st years old.

Dj.sommie: Kizungu na watu wat z ni kama zakayo na ukweli.. ruto must go.

Iamkarenju: Diamond mastered how to get Kenyans attention.

Si mara ya kwanza kwa kiingereza cha Diamond kujadiliwa mitandaoni. Katika siku za nyuma, amesikika akitumia Kiingereza kibovu mara kadhaa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved