Diana Marua apigwa na butwaa baada ya Milly Chebby kufichua wanaume amewahi kulala nao

“Tukisema mimi na Terence tunahama. Mimi na Terence tunaenda,” Diana Marua alisema.

Muhtasari

•Milly Chebby aliweka wazi kuwa Terence Creative ndiye mwanaume wa saba ambaye alishiriki naye tendo la ndoa.

•Mkewe Bahati, Diana Marua alitakiwa kumtaja mpenzi wake wa zamani ambaye akipewa nafasi angerudiana naye.

Terence Creative na mkewe Milly Chebby
Image: INSTAGRAM

Wanandoa mashuhuri wa Kenya The Bahati’s (Bahati & Diana Marua) na The Mwangi’s (Terence Creative & Milly Chebby) walishiriki katika mchezo wa wanandoa unaojulikana kama Truth or Dare.

Katika mchezo huo uliopakiwa kwenye chaneli ya YouTube ya Diana Marua mnamo Jumanne, mastaa hao wanne walihitajika kufunguka kuhusu ukweli fulani kuhusu maisha yao au kuagizwa kufanya kitu fulani maalum.

Wakati mchezo ukiendelea, mke wa Terence, Milly Chebby alijikuta kwenye nafasi ngumu ambapo alihitajika kufichua idadi ya watu aliowahi kushiriki nao mapenzi maishani.

"Saba, saba!" Milly Chebby alijibu baada ya kushangazwa na swali hilo aliloulizwa na mume wake Terence.

Diana Marua ambaye alikuwa ameketi kando yake alionekana kushtushwa sana na jibu lake na kuomba ufafanuzi zaidi kutoka kwake ikiwa Terence ndiye alikuwa mwanaume wa 7.

“Tukisema mimi na Terence tunahama. Mimi na Terence tunaenda,” Diana Marua alisema.

Milly aliweka wazi kuwa Terence ndiye mwanaume wa saba ambaye alishiriki naye tendo la ndoa.

Terence Creative ambaye alikataa kufichua idadi ya watu ambao amefanya nao mapenzi maishani hata hivyo alionekana kutilia shaka jibu ambalo mkewe alitoa.

Alidai kuwa yeye binafsi alihesabu wanaume wanane ambao mkewe aliwahi kumtajia na hata kutaja baadhi ya wanaume ambao mama huyo wa mtoto wake mmoja aliwahi kumtajia. Wapenzi hao hata hivyo walikubaliana kwamba kati ya wanaume hao kulikuwa na mwanamume ambaye aliwahi kushiriki mchezo wa kitandani na Milly msituni, dereva wa matatu na daktari.

“Terence, nina jina na wateja wa kuwahifadhi,” Milly alimwambia mumewe huku akiendelea kuhesabu.

Mwingine ambaye alijikuta kwenye nafasi ngumu ni Diana Marua ambaye alitakiwa kumtaja mpenzi wa zamani ambaye akipewa nafasi angerudiana naye.

Katika majibu yake, mama huyo wa watoto watatu alibainisha kuwa wapenzi wake wa zamani walimfanyia mambo mabaya na hatataka kurudiana na yeyote kati yao.

"Wapenzi wangu wa zamani walinifanyia machafu, kwa hivyo nisingependa kurudi tena. Walinifanyia vibaya na babe unajua. siwezi. Huo ndio ukweli wangu. Hakuna mwenye mzuri,” Diana Marua alisema.

Terence Creative kwa upande wake aliagizwa kumpigia simu mpenzi wake wa zamani na kumwambia kuwa anampeza, jambo ambalo alifanya lakini akakata simu mara baada ya kusikia sauti ya mwanamke na ya mtoto upande wa pili wa simu.

Bahati aliulizwa ni mara ngapi huwa anajiridhisha mwenye kimapenzi wakati mke wake Diana Marua hayupo. Katika majibu yake, alisema kuwa hajawahi kujiridhisha tangu aingie kwenye mahusiano na Diana.

Mastaa hao pia walikubaliana kuwa wote hawawezi kuwaruhusu wapenzi wao kulala na rafiki yao wa karibu kwa dola milioni moja (Ksh 147milioni).