Hachomoki pale mpaka kifo! Zuchu adaiwa kumroga Diamond Platnumz

Pimbi alisema Diamond sasa ametulia na hawezi kutoka nje ya mahusiano yake na Zuchu

Muhtasari

•Pimbi alisema Zuchu ameweza kumshika Diamond  walikoshindwa kumshika wapenzi wake wote wa zamani.

•Alisema kwamba Diamond sasa ametulia na hawezi kutoka nje ya mahusiano yake na malkia huyo kutoka Zanzibar.

Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Diamond na msanii wake Zuchu ambaye anadaiwa kuwa kwenye mahusiano naye
Image: KWA HISANI

Malkia wa Bongo Zuchu amefanikiwa kweli kweli kuuteka moyo wa bosi wake Diamond Platnumz, mchekeshaji Mr Pimbi amesema.

Pimbi ambaye anadai kwamba ana uwezo wa kuona mbele amesema binti huyo wa staa wa taarabu Khadija Kopa ameweza kumshika Diamond  walikoshindwa kumshika wapenzi wake wote wa zamani.

"Zuchu amefanikiwa kushika sharubu za Simba bila silaha yoyote. Sharubu ambazo zilimshinda Wema Sepetu, sharubu ambazo zilimshinda Zari the Boss Lady, sharubu ambazo zilimshinda Tanasha Donna, zilizomshinda mheshimiwa Jokate, ni sharubu ambazo zimewashinda watu wengi sana wakubwa na warembo. Kale katoto kako simple lakini hatari," Pimbi alisema katika mahojiano na Mbengo TV.

Mchekeshaji huyo mbilikimo alidai kwamba Zuchu amemfanyia bosi huyo wa WCB "urogi mzuri" na kumkoroga akili.

Kulingana naye, Diamond sasa ametulia na hawezi kutoka nje ya mahusiano yake na malkia huyo kutoka Zanzibar.

"Diamond hatotoka kwa Zuchu mpaka kufa. Maona yangu yananionyesha Diamond ameshakula pingu za maisha mpaka kifo. Hiyo ndo break na hatachomoka.. Alikuwepo pale Wema, hakufanikiwa kumvuruga Diamond Platnumz akili hivo. Diamond alipokuwa na Wema bada alikuwa na skendo za wanawake wengine. Alipokuwa na Zari bado alikuwa na skendo za wanawake wengine mpaka anacheat na Hamisa Mobetto na anazaa naye. Alipokuwa na Tanasha Donna, dakika mbili tu mapenzi yamekwisha. Lakini Zuchu amefanikiwa kumpiga kabali," Alisema.

Pimbi alidai kwamba Diamond na Zuchu wamekuwa kwa mahusiano kwa zaidi ya miaka miwili tayari.

Aidha alimpongeza Bi Khadija Kopa kwa jinsi alivyomfunza bintiye na kufanikisha mahusiano yake na Diamond.

Hivi majuzi Diamond aliwasisimua wanamitandao kwa kujitambulisha kama 'mume wa Zuuh' kwenye Instagram. 

Diamond alikuwa akicomment kuhusu video iliyomuonyesha akitumbuiza mashabiki wake nchini Ureno ambayo ilipakiwa kwenye ukurasa rasmi wa WCB.

"Huyo ni mume wa Zuuh," Diamond aliandika.

Zuchu hata hivyo alionekana kupingana na ujumbe huo wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji Ankali Mambi.

Alidai kwamba hakuona comment hilo la bosi wake na hata kuzua shaka ikiwa kwa kweli ni yeye alitajwa.

"Zuuh wako wengi. Ni kweli naitwa Zuuh lakini si Zuuh mimi, kama ingekuwa mimi angeniambia. Itakuwa Zuuh mwingine," Zuchu alisema.

Mtunzi huyo wa kibao 'Sukari'  alisistiza kuwa uhusiano wake na Diamond ni wa kikazi tu wala sio mahusiano.