"Hakuna kutumia P2 tena!" Ex wa Harmonize, Kajala afichua mpango wa kupata mtoto wa pili

Muigizaji huyo anadai sasa ni wakati mwafaka wa yeye kupata mwingine.

Muhtasari

•Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alifichua kwamba hatatumia tena dawa za kuzuia mimba kuendelea.

•Wakati wa mahusiano yake na Harmonize mwaka jana, Kajala alidaiwa kutungwa ujauzito na mwimbaji huyo mahiri.

amefichua mpango wa kupata mtoto wa pili
Muigizaji wa Bongo Kajala Masanja amefichua mpango wa kupata mtoto wa pili
Image: INSTAGRAM// KAJALA MASANJA

Muigizaji mkongwe wa filamu Bongo Frida Kajala Masanja amedokeza kuwa yuko tayari kupata mtoto wake wa pili.

Mpenzi huyo wa zamani wa staa wa Bongofleva Harmonize anadai sasa ni wakati mwafaka wa yeye kupata mwingine.

"Nadhani sasa ni muda sahihi wa kupata mdogo wako dada Pau (Paula)," aliandika kwenye Instastori zake.

Ujumbe huo unaonekana kuelekezwa kwa bintiye wa pekee Paula Paul ambaye alimleta duniani takriban miongo miwili iliyopita.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 aliendelea kufichua kwamba hatatumia tena dawa za kuzuia mimba kuendelea.

"Hakuna kutumia P2 tena, niko tayari kuwa mama tena," alisema.

Kajala hakufichua kama tayari yuko kwenye mahusiano mengine baada ya kumtema Harmonize mwishoni mwa mwaka jana.Ujumbe wake hata hivyo inaibua shaka dhana kuwa huenda tayari kuna mwanaume mwingine katika maisha yake.

Mama huyo wa binti mmoja alitangaza kutengana na Harmonize mwezi Desemba baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takriban miezi minane. Wawili hao walikuwa wamerudiana mwezi Mei baada ya Harmonize kuomba msamaha.

"Mimi kama mwanamke na binadamu nimeumbwa kupenda na kusamehe pia, ila kwenye hili nastahili kuchekwa, nastahili kubezwa na kudharauliwa pia. Sipo hapa kujitetea wala kutia huruma ni kweli nilifanya makosa na nimeyagundua makosa yangu, mimi siyo mkamilifu," Kajala alisema Desemba 2022  kupitia Instagram.

Aliongeza, "Hakika nimekosea familia yangu, ndugu zangu, na marafiki zangu. Kutenda kosa si kosa, kosa kurudia kosa. Namsemehe X wangu na niko tayari kuenda kwa hatua nyingine."

Wakati wa mahusiano yake na Harmonize mwaka jana, Kajala alidaiwa kutungwa ujauzito na mwimbaji huyo mahiri.

Madai kuwa alikuwa mjamzito yaliibuka baada ya yeye kuchapisha video iliyomuonyesha akiwa hospitalini. Video aliyochapisha mapema mwezi Novemba ilionyesha sindano iliyodungwa kwenye mkono wake.

Baadae ilibainika kwamba muigizaji huyo alikuwa akiugua baada ya aliyekuwa mpenziwe, Harmonize kumtakia afueni ya haraka.

Pona haraka mpenzi. Siwezi kusubiri kukuona ukiwa mwenye nguvu tena," staa huyo wa Bongo aliandika chini ya picha ya Kajala akionekana mdhaifu ambayo alipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kajala ana binti wa miaka 20, Paula Paul Kajala kutoka kwa ndoa yake ya zamani na mtayarishaji wa muziki P Funk Majani.