Harmonize amnunulia Kajala Range Rover nyingine, asema anataka kumfanya mwanamke ghali

Muhtasari

•Bosi huyo wa Konde Music Worldwide amesema anataka Kajala awe na magari mawili kwa kuwa pia yeye anamiliki mawili.

•Konde Boy pia amepuuzilia mbali madai kuwa hatua yake kumnunulia Kajala gari aina ya Range Rover ni kiki.

Harmonize na Kajala Masanja
Harmonize na Kajala Masanja
Image: HISANI

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amefichua kuwa tayari ameshaagiza gari lingine kwa ajili ya aliyekuwa mpenzi wake Fridah Kajala Masanja.

Harmonize ambaye wiki za hivi majuzi amekuwa akijaribu njia tofauti kumshawishi Kajala warudiane amesema gari hilo aina ya Range Rover litawasili siku ya Ijumaa.

"La pili siku ya Ijumaa. Lile jeusi kutoka Afrika Kusini tunalipia ushuru Goma, linakuja kupaki hapa. Kwa hivyo atakuwa na Range Rover mbili . ROVA demu wamuuni tuu sio kigogo Walekelini wala sio mke wa Laiza mchimba madini," Harmonize ametangaza kupitia Instagram.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide amesema anataka Kajala awe na magari mawili kwa kuwa pia yeye anamiliki mawili.

Amesema lengo lake ni kumfanya muigizaji huyo kuwa mwanamke ghali ambaye ataheshimika na wapenzi wake wote wa zamani.

"Niko na VX nyeupe na nyeusi kwa hivyo na yeye anaenda kuwa na mbili pia. Usafiri wa familia ulioje. Nataka nikufanye ghali mpaka maex waanze kukuita bosi washike na adabu bosi lady Kajala," Amesema.

Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Konde Boy pia amepuuzilia mbali madai kuwa hatua yake kumnunulia Kajala gari aina ya Range Rover ni kiki.

Amesisitiza kuwa gari ambalo alionyesha alimnunulia muigizaji huyo mwezi uliopita bado lipo na kilichobaki ni yeye kurudi aanze kulitumia.