Harmonize atoa onyo kali kwa mpenzi wa Hamisa Mobetto, ajigamba kuwa tajiri zaidi yake

Harmonize amemtaka Kevin amnunulie Hamisa nyumba ili kudhihirisha kuwa yeye ni tajiri sana kama inavyodaiwa.

Muhtasari

•Harmonize amejipiga kifua kuwa yeye ni tajiri kuliko mpenzi wa rafiki yake Hamisa Mobetto, Kevin Sochax.

•Wakati huo huo, Harmonize alisisitiza kuwa mpenzi huyo wa zamani Diamond ni rafiki yake tu na si mpenzi wake.

Harmonize ametupa vijembe kwa mumewe Hamisa Mobetto
Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo, Rajab Abdul Kahali maarufu Harmonize amejipiga kifua kuwa yeye ni tajiri kuliko mpenzi wa rafiki yake Hamisa Mobetto, Kevin Sowax.

Wakati akijibu madai ya mtangazaji Juma Lokole kwamba hawezi kushindana na Kevin katika masuala ya fedha, Konde Boy alisema kuwa mifuko yake imesheheni zaidi ya Mtogo huyo.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidokeza kuwa njia mojawapo ya kulinganisha utajiri wao ni kuangalia aina ya gari kila mmoja anamiliki.

“Ingawa mimi sio mtu wa kuongelea maisha ya watu nisiowajua lakini niamini niko na hela nyingi kuliko jamaa huyo. Kabla hujamnunulia mwanamke gari inatakiwa tujue unaendesha gari ganii!! Au ndio hayanihusu. Si tushavuka kwenye magari,” Harmonize alisema katika taarifa kwenye Instastori zake.

Ili mfanyibiashara huyo wa Togo kudhihirisha kuwa yeye ni tajiri sana kama inavyodaiwa, Harmonize amemtaka amnunulie Hamisa nyumba.

"Kama hawezi, basi nitamuonyesha jinsi tulivyo serious na marafiki zetu wakubwa, sisi wanaume wa Kitanzania!! Kwenye magari tushavuka,” alisema.

Wakati huo huo, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alisisitiza kuwa mpenzi huyo wa zamani Diamond Platnumz ni rafiki yake tu na si mpenzi wake.

Hivi majuzi, Hamisa Mobetto alikanusha madai ya kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Harmonize.

Kwenye mahojiano na Rick Media, mpenzi huyo wa zamani wa Diamond Platnumz alibainisha kuwa hakuna chochote kikubwa kati yake na Konde Boy na kubainisha kuwa mwimbaji huyo wa kibao ‘Single Again’ ni rafiki yake tu.

“Yeye ni rafiki tu. Hakuna zaidi, hakuna kidogo, "alisema.

Baada ya kubainishiwa kuwa Harmonize anayapenda sana makalio yake makubwa, mama huyo wa watoto wawili alikiri kuwa hafahamu hilo.

Wiki chache zilizopita, Harmonize alimtambulisha aliyekuwa mpenzi wake, Hamisa Mobetto kama rafiki wake wa karibu almaarufu BFF.

Harmonize alianza kwa kupakia picha ya Hamisa Mobetto ambayo inamuonesha akiwa ameketi kwenye ndege, kwenye viwiko amepakata mto na viganjani ameshikilia simu kwa tabasamu akiwa kama anatumiana ujumbe na mtu.

“Kutana na BFF wangu mpya,” Harmonize aliandika.

Hamisa Mobetto naye si mchache. Aliichukua picha hiyo kutoka kwa Instastory ya Harmonize na kuichapisha kwenye ukurasa wake na kuandika “BFF” kisha kuiambatanisha na emoji za makopa ya mapenzi.