Hatimaye mpenzi wa Ex wa Eric Omondi atiwa mbaroni kwa madai ya kumdhulumu

Muhtasari

•Nicola alikamatwa Jumatatu mchana baada ya mpenzi wake kumshtumu kwa kumshambulia Ijumaa asubuhi.

•Jumapili Chantal alimwagiza mpenziwe ajisalimishe katika kituo cha polisi huku akifichua kuwa hajulikani alipo.

Nicola, Chantal na Eric Omondi
Nicola, Chantal na Eric Omondi
Image: INSTAGRAM

Polisi wanamzuilia mfanyibiashara Nicola Traldi kwa madai ya kumdhulumu mpenzi wake Chantal Grazioli.

Nicola alikamatwa Jumatatu mchana baada ya mpenzi wake kumshtumu kwa kumshambulia Ijumaa asubuhi.

Mchekeshaji Eric Omondi na ambaye ni mpenzi wa zamani wa Bi Chantal ndiye aliyetangulia kufichua yaliyompata kipusa huyo mwenye asili ya Italia.

"Nilipata Chantal amevunjika mguu. Alikuwa amenyongwa kwa shingo. Alikuwa ameangushwa kwa ngazi. Vitu vilikuwa vimepasuka. Ni mlinzi, majirani na caretaker ambao walimsaidia," Eric alisimulia katika mahojiano na Eve Mungai.

Eric alieleza kuwa alimpeleka mpenzi huyo wake wa zamani hospitalini na kumsaidia kupiga ripoti katika kituo cha polisi.

Jumapili Chantal alimwagiza mpenziwe ajisalimishe katika kituo cha polisi huku akifichua kuwa hajulikani alipo.

" Iwapo anadai kuwa anasingiziwa kwa nini asijipeleke kwenye kituo cha polisi? Hapatikani ata," Nicola alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Video iliyofikia Radio Jambo Jumatatu ilionyesha Nicola akiwa katika kituo cha polisi cha Thindigua ambako anaripotiwa kuzuiliwa.

Mfanyibiashara huyo alionekana akiwa amesimama mbele ya kituo hicho huku akiwa amejifunika sura kwa kofia.

Haya yalijiri masaa machache tu baada ya Chantal kudai kuwa maisha yake yamo hatarini. Alieleza kuwa baada ya mpenziwe kumshambulia alitishia kurudi baadae ili kuendelea kumpiga.

Aidha mpenzi huyo wa zamani wa Eric alidai kuwa hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mpenziwe kumdhulumu.

"Mara nyingi ameniagiza nijiepushe na vyombo vya habari, jambo ambalo nilifanya kwa kuhofia kudhalilishwa na kushambuliwa. Niliogopa kujitokeza lakini siku ya Ijumaa ikiwa mbaya zaidi, nilijaribu kumfikia mama yangu bila mafanikio, wakati huo huo majirani zangu, walinzi na caretakeri walikuja kuniokoa," Chantal alisema.

Alisema Eric ndiye alimsaidia kufunguka kuhusu yale ambayo amekuwa akipitia katika mahusiano yake.