'Hatujawahi kuwa marafiki!' Amber Ray afunguka uhusiano wake na aliyekuwa mke mwenzake Amira

Mwanasoshalaiti huyo alidokeza kuwa hakuna wakati ambapo kutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na mkewe Jimal.

Muhtasari

•Amber Ray amebainisha kuwa yeye na mama huyo wa watoto wawili hawajawahi kuwa marafiki kamwe.

•Alidokeza kuwa hakuna wakati ambapo kutakuwa na uhusiano mzuri kati yake na mke huyo wa Jimal.

Image: INSTAGRAM// AMBER RAY/ AMIRA

Mwanasoshalaiti Faith Makau almaarufu Amber Ray ameweka wazi kuwa mke wa Jimal Rohosafi, Amira sio adui wake.

Amber Ray hata hivyo amebainisha kuwa yeye na mama huyo wa watoto wawili hawajawahi kuwa marafiki kamwe.

"Mimi na Jamal ni marafiki bado, hakuna zaidi ila marafiki tu. Kuhusu mkewe, hatujawahi kuwa marafiki, yeye sio adui wangu pia," Alisema katika kipindi cha As It Is kwenye YouTube channel yake.

Mama huyo wa mvulana mmoja alikuwa akishiriki mazungumzo na Shicco Waweru ambapo alijibu maswali kuhusu maisha yake.

Alidokeza kuwa hakuna wakati ambapo kutakuwana uhusiano mzuri kati yake na mke huyo wa aliyekuwa mpenziwe.

"Mwisho wa siku, nilikuwa na mahusiano na Jamal. Ni jambo ambalo hatawahi kukubali. Lakini kilichofanyika kilifanyika. Sijawahi kutaka kuongea kumhusu," Alisema.

Alimshutumu mke mwenza huyo wake wa zamani kueneza uongo dhidi yake na kubainisha kuwa tayari amesonga mbele na maisha yake. 

"Chochote kilichowahi kutokea huko nyuma ni historia kwangu. Tayari nimesonga mbele na maisha yangu na nipo mahali pa amani sana," Alisema.

Mwaka jana, drama zisizoisha zilikumba ndoa ya Mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki Matatu jijini Nairobi Jimal Rohosafi baada ya kumtambulisha Amber Ray kama mke wake wa pili.

Amira ambaye ni mke wa kwanza wa Jimal alionekana kutokubali wazo la mumewe kuoa mke mwingine na hivyo kuwa na vita visivyoisha na mwanasholaiti huyo kwa miezi kadhaa ambayo walikuwa wake wenza.

 

Kufikia sasa wawili hao tayari wametengana na mfanyabiashara huyo ambaye sameachwa akijaribu kujenga upya ndoa yake na Amira.