logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hongera! Mwanasoshalaiti Vera Sidika anatarajia mtoto wa pili na Brown Mauzo

Vera alifichua kwamba amekuwa mjamzito kwa takriban miezi saba sasa.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri19 December 2022 - 11:55

Muhtasari


•Vera alifichua kuwa anatarajia mtoto wake wa pili na mumewe Brown Mauzo siku ya Jumatatu kupitia mtandao wa Instagram.

•Alifichua  alikuwa akipanga kuenda nje ya nchi ili kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti wakati alipogundua kuwa ni mjamzito.

Mwanasoshalaiti Vera Sidika ni mjamzito kwa mara nyingine, takriban mwaka mmoja baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Vera alifichua kuwa anatarajia mtoto wake wa pili na mumewe Brown Mauzo siku ya Jumatatu kupitia mtandao wa Instagram.

Katika tangazo lake, mama huyo wa binti mmoja alifichua kwamba amekuwa mjamzito kwa takriban miezi saba sasa.

"Wapendwa, ndugu wa Asia yuko njiani!!!🎊💃🏼Mungu alikuwa na mipango ya familia yetu ndogo kukua zaidi 🙏  Tuliegundua tukiwa na miezi 4 na nusu," alisema.

Vera aliambatanisha ujumbe huo wake na picha inayomuonyesha akiwa ameshikilia tumbo lake kubwa lililochomoza.

Alifichua alikuwa akipanga kuenda nje ya nchi ili kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti wakati alipogundua kuwa ni mjamzito.

"Ilinibidi kufuta safari yangu na kukumbatia muujiza wetu mdogo 😍🎊Nimejifunza kwamba kuwa mjamzito inamaanisha kuwa kila siku ni siku nyingine karibu na kukutana na mpenzi mwingine wa maisha yetu," alisema.

Kufuatia hilo, mwanasoshalaiti huyo ametoa shukrani za dhati kwa mumewe kwa kufanikisha ujauzito wa pili.

Aidha, alieleza furaha yake kubwa kuona kuwa bintiye mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili atapata ndugu hivi karibuni.

"Nimefurahi sana kwamba Asia anapata ndugu ambaye atakua naye. BFF inapakia 💃🏼,"

Brown Mauzo kwa upande wake alimshukuru mwanasoshalaiti huyo kwa kuwa mke bora kwake na mama mzuri kwa mtoto wao, Asia Brown.

Mwanamuziki huyo alimhakikishia Vera kuhusu upendo wake mkubwa kwake na kukiri kuwa anafurahia hatua mpya katika ndoa yao.

"Ni baraka iliyoje!!! Mtoto wa pili ako njiani 🤰❤️Tunapokaribia hatua nyingine katika ndoa yetu, ninachotaka kusema ni asante kwa kuwa mke na mama bora. Wewe ni zawadi kutoka kwa ulimwengu, na nina bahati kuwa na wewe katika maisha yangu. Nakupenda mke wangu @queenveebosset," alisema.

Wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka miwili na walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza Oktoba mwaka jana.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved