Inapendeza! Bintiye Diamond amkumbatia kwa upendo babake wa kambo, waonyesha uhusiano mzuri

Zari alionekana kufurahishwa sana na uhusiano mzuri ulioonyeshwa kati ya mumewe Shakib na bintiye.

Muhtasari

•Tiffah ambaye ni mtoto wa kwanza wa Zari na Diamond alionekana akimkimbilia Shakib alipokuwa akishuka kwenye gari lake.  

•Punde baada ya malkia huyo wa miaka 8 kufika pale alipokuwa Shakib, alimkumbatia vizuri na kumuinua kwa mikono miwili.

akimkumbatia Shakib.
Tiffah Dangote akimkumbatia Shakib.
Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Siku ya Jumapili jioni, mwanasosholaiti na  mfanyibiashara maarufu wa Uganda Zari Hassan alishiriki video nzuri ya mumewe Shakib Cham Lutaaya akikaribishwa nyumbani na binti yake Tiffah Dangote kwa njia ya kupendeza sana. 

Katika video hiyo ambayo Zari alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, Tiffah ambaye ni mtoto wa kwanza wa mwanasosholaiti huyo na staa wa Bongo Diamond Platnumz alionekana akimkimbilia Shakib alipokuwa akishuka kwenye gari lake.  

Punde baada ya malkia huyo wa miaka minane kufika pale alipokuwa Shakib, babake huyo wa kambo alimkumbatia vizuri na kumuinua kwa mikono miwili. Wawili hao kisha walionekana kuwa na mazungumzo mafupi nje ya gari.

Zari alionekana kufurahishwa sana na uhusiano mzuri ulioonyeshwa kati ya mumewe huyo mwenye umri wa miaka 32 na bintiye. Aliambatanisha video yake na wimbo “I love you baby” wa Emilee.

Hii sio mara ya kwanza kwa uhusiano mzuri kati ya Shakib na bintiye Zari kuonekana wazi.

Siku chache baada ya Zari na Shakib kufunga pingu za maisha mwaka jana, video ya kusisimua ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 31 akiwa amekaa kwenye sofa huku Tiffah akiwa amelala mapajani mwake.

Wawili hao walionekana kutazama sinema kwenye Televisheni.

Mwezi uliopita, Shakib alimsherehekea mtoto wake mwingine wa kambo Riaz Nasibu Abdul almaarufu Prince Nillan katika siku yake maalum.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 alitumia mitandao ya kijamii kumsherehekea mtoto wa mwisho wa mwanaosholaiti huyo alipokuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa. Prince Nillan alifikisha umri wa miaka saba Jumatano, Desemba 7.

Shakib alichapisha video nzuri iliyoonyesha akitembea bega kwa bega na Prince Nillan huku wakiwa wamevalia suti za kijivu zinazolingana.

"🎂🎁🙏🏻" aliandika kwenye video hiyo.

Katika video hiyo, wanaume hao wawili walionekana wakitembea pamoja huku tabasamu zuri likionekana kwenye nyuso zao.

Shakib ambaye pia aliadhimisha siku yake ya kuzaliwa mapema mwezi Disemba anaonekana kuwa na uhusiano mzuri na watoto wa Zari Hassan. Mwanasoshoaliti huyo ambaye anaishi Afrika Kusini ana watoto watano ambao alizaa na wapenzi wawili wa zamani, Ivan Ssemwanga na Diamond Platnumz.

Mfanyibiashara huyo na mama huyo wa watoto 5 walifunga ndoa rasmi mwezi Oktoba baada ya kuchumbiana kwa zaidi ya mwaka mmoja.