Ishara nzuri huku ex wa Bahati, Yvette Obura akitumia wimbo wake kujigamba na umbo wake mzuri (+video)

Mama Mueni alichagua kutumia wimbo wa mzazi huyo mwenzake ‘Wanani’ kujigamba kuhusu mwili wake.

Muhtasari

•Mama Mueni aliuonyesha kwa fahari umbo mzuri wa mwili wake huku akizungukazunguka ndani ya jumba kubwa tupu.

•Mwili wake mzuri kando, kilichoonekana kuwasisimua wengi ni chaguo lake la wimbo wa kuambatanisha na video aliyochapisha.

Image: INSTAGRAM// YVETTE OBURA

Siku ya Jumapili, mzazi mwenza wa mwimbaji Bahati, Bi Yvette Obura alionyesha mwili wake mzuri katika video ya takriban dakika moja na nusu ambayo alichapisha kwenye mtandao wa Instagram.

Katika video hiyo, mama huyo wa binti mmoja aliuonyesha kwa fahari umbo mzuri wa mwili wake huku akizungukazunguka ndani ya jumba kubwa tupu.

"Video nasibu: Siku katika maisha yangu nikifanya kazi na vyumba vya @home_sweet_home. Asante @_mjukuu kwa video. HELLO HAPPY WEIGHT,” Yvette Obura aliandika chini ya video ambayo alipakia.

Mwili wake mzuri kando, kilichoonekana kuwasisimua wanamitandao ni chaguo lake la wimbo wa kuambatanisha na video aliyochapisha.

Mrembo huyo ambaye ana mtoto mmoja msichana na Bahati anayefahamika kwa jina Mueni Bahati alichagua kutumia wimbo wa mapenzi wa mzazi huyo mwenzake ‘Wanani’ kujigamba kuhusu mwili wake.

"Umeshukia toka binguni. Wee ni malaika. Au Nakosea.Sifa zote tumpee manani., Aliyekuumba hajakose…Toto si toto, uuh lala. Nimeshinda lotto, uuh lala. Figure moto, uuh lala. Toto si toto, uuh lala. Nimeshinda lotto, uuh lala. Kukupata mtoto, uuh lala,” ndio maneno ya wimbo ambao Yvette  alitumia.

Wimbo huo unaendelea, “Basi wewe wanani. Niambie wanani, wanani. Kama sio wangu tuu (x2)…I heard i like you. But i love you. Yes it’s true yes its true.. And if they ask me to choose, Between me and you, Baby i’ll choose you, Cause i’m you uhh uhh..”

Hii huenda ni dokezo nzuri kwamba mfanyibiashara huyo hana kinyongo na mpenzi huyo wake wa zamani na kwamba anashabikia muziki wake.

Katika kipindi cha miezi kadhaa ambayo imepita, Yvette na mkewe Bahati, Diana Marua hata hivyo wamedaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri.

Mwezi Machi hata hivyo, Diana alipuuzilia mbali tetesi hizo na kuweka wazi kuwa hana ugomvi wowote na mzazi mwenza huyo wa mumewe.

"Sina tatizo na huyo mama. Niliona nyie mkiuliza na kukaibuka vichwa vya habari vya hapa na pale kwa sababu ya chapisho nililoweka, sina ugomvi na mtu yeyote ni vile labda hatujapata wakati wa kupata kuzungumza.

Hakuna kutoelewana kwamba tuna chochote kwa hivyo ambacho kilitafsiriwa vibaya na ningependa kuiweka hapa tena kwamba hakuna beef kati yangu na mama Mueni. Tuko tu katika nafasi ambayo tuko hivi sasa,"Alisema Diana.

Hapo awali, wawili hao walikuwa na uhusiano mzuri sana na walionekana pamoja mara nyingi, jambo ambalo halionekani siku hizo na hivyo kuzua tetesi za kukosana.