Justina Syokau afichua kwa nini alitazama filamu ya watu wazima mara ya kwanza baada ya kuolewa

Mwimbaji huyo amefichua kuwa ni baada ya kuingia kwenye ndoa ambapo alitazama filamu yake ya kwanza ya watu wazima.

Muhtasari

•Justina alidai kuwa alishauriwa kuwa kutokuwa bora kitandani kungeweza kuwa sababu ya mume wake kuenda nje ya ndoa.

•Justina alifichua baada ya ndoa yake kukumbwa na matatizo, aliachana na mumewe na tangu wakati huo amekuwa hapendi wanaume.

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau
Image: HISANI

Mwimbaji wa nyimbo za Injili mwenye utata Justina Syokau amefichua kuwa ni baada ya kuingia kwenye ndoa ambapo alitazama filamu yake ya kwanza ya watu wazima.

Katika mahojiano ya hivi majuzi na Oga Obinna, mwimbaji huyo wa kibao ‘Twedi Twedi’ aliweka wazi kwamba alikuwa akijaribu kumfurahisha mume wake kwenye masuala ya kitandani alipotazama filamu hizo kwa mara ya kwanza.

Alidai kuwa alishauriwa kuwa kutokuwa bora kitandani kungeweza kuwa sababu ya mume wake kuenda nje ya ndoa na hivyo alikuwa na hamu ya kuimarika.

“Niliangalia nione, labda ni mitindo sijui. Juu nilikuwa nimeokoka hiyo miaka yote. Labda sijui mitindo ya kumpea,” Justina Syokau alisema.

Aliongeza, “Niliambiwa na watu, labda sijui kumpatia vizuri, ndio sababu anatembea nje. Nikaenda nikaambiwa video ndizo hizi angalia hapa. Nikakuta niko sawa ata kuliko hao.”

Mwimbaji huyo aliyezingirwa na dram nyingi hata hivyo alibainisha kuwa kutazama filamu za watu wazima kulimwacha tu bila suluhu kwani aligundua kuwa alikuwa bora zaidi kuliko wahusika. Alibainisha kuwa uaminifu unapokosa katika ndoa, mtu aliyeathiriwa mara nyingi huhisi labda hawamridhishi mwenza wake kitandani.

Justina alifichua kuwa baada ya ndoa yake kukumbwa na matatizo tele, baadaye aliachana na mumewe na amekuwa hapendi wanaume tangu wakati huo.

"Imekuwa miaka 10 bila tendo la ndoa. Ninaogopa wanaume. Ninaogopa sana wanaume. Nazungumza sana kuhusu wanaume, watu wanadhani napenda wanaume, nahitaji wanaume, lakini HAPANA,” alisema.

Aliweka wazi kuwa wanaume wote ambao ameonekana nao kwenye video ni wahusika tu..