logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kabla ya kushiriki mapenzi, huwa namuomba Mungu ampe nguvu DJ Mo ili nifurahie! -Size 8 afichua ya kitandani

"Akikuja huwa namshika nasema 'Baba katika jina la Yesu' (Huwa hajui). Huwa naambia Mungu ampatie nguvu nataka kujibamba," alisema.

image
na Radio Jambo

Makala25 March 2023 - 12:09

Muhtasari


•Size 8 amefichua kwamba huwa anasali kwa Mungu kabla ya kushiriki mchezo wa kitandani na mumewe Samuel Muraya almaarufu DJ Mo.

•Size 8 aliweka wazi kwamba huwa anaomba mumewe aweze kumridhisha ili asiwahi kupatwa na fikra za kuenda nje ya ndoa.

Mwimbaji huyo amezindua kanisa lake.

Mwimbaji na mhubiri mashuhuri Linet Munyali almaarufu Size 8 amefichua kwamba huwa anasali kwa Mungu kabla ya kushiriki mchezo wa kitandani na mumewe Samuel Muraya almaarufu DJ Mo.

Akizungumza kwenye chaneli ya YouTube ya Diana Chacha, mama huyo wa watoto wawili alifichua kwamba mara kwa mara yeye huomba ili apate hamu ya kufanya mapenzi wakati  mumewe anapotaka lakini hajisikii tayari.

Size 8 amefichua kwamba huwa anasali kwa Mungu kabla ya kushiriki mchezo wa kitandani na mumewe Samuel Muraya almaarufu DJ Mo.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili pia alifichua kwamba kabla ya kuingia kwenye mchezo huo, yeye kawaida humwombea DJ Mo apate nguvu za kumridhisha kama ambavyo angetaka.

"Akikuja huwa namshika nasema 'Baba katika jina la Yesu' (Huwa hajui). Huwa naambia Mungu ampatie nguvu nataka kujibamba," alisema.

Mhubiri huyo alibainisha kuwa huwa anafanya maombi hayo bila ya mumewe kujua.

"Huwa naomba kimoyomoyo namwambia Mungu ,' Mungu Baba patia huyu mwanaume nguvu, wewe ndiye uliumba tendo hili, Baba jinsi ulivyoliumba,nataka kulifurahia jinsi ambavyo uliona," alisema.

Size 8 aliweka wazi kwamba huwa anaomba mumewe aweze kumridhisha ili asiwahi kupatwa na fikra za kuenda nje ya ndoa.

Wakati mkewe akiendelea kufunguka ya kitandani, DJ Moh alibainisha kwamba  huwa hajui mkewe anaombea nini.

Aidha, alidokeza kuwa wakati akielekea nyumbani, pia yeye hufanya ombi kwa Mungu akimsihi awape kipindi kizuri.

"Wakati akiomba na mimi nikiwa kwa gari huwa nasema atajua mimi ni nani," alisema.

Wanandoa hao waliwashauri wapenzi wengine kumshirikisha Mungu kila wakati wanaposhiriki tendo la ndoa.

"Watu hucheka wakiambiwa ati waombe kabla ya mapenzi. Yeye (DJ Mo) hajui, lakini mimi kwa upande wangu huomba," alisema.

Takriban mwezi mmoja uliopita wawili hao waliandamana na watoto wao hadi jijini Dubai ambako waliadhimisha siku ya kuzaliwa ya DJ Mo.

Huku akiadhimisha siku hiyo maalum katika maisha yake, Mo alielezea furaha yake kubwa kwa kuweza kuisherehekea na familia yake.

"Kheri ya kuzaliwa kwangu!! Ni siku yangu leo, nashukuru Mungu nimesherehekea na familia yangu Dubai," alisema siku ya Jumapili.

Mcheza santuri huyo alifichua kwamba ilikuwa ndoto yake na bintiye, Ladasha Wambui, kuzuru jiji la Dubai na kujionea mandhari yake ya kuvutia.

Alichapisha video inayomuonyesha akijivinjari na familia yake kwenye ufukwe wa bahari jijini humo na kufurahia safari ya jahazi.

"Ndoto imetimia!!!!! Siku ya kuzaliwa jijini Dubai katika Jahazi na mke. Wakati wa ufukweni na shughuli nyingi pia zilikuwa sehemu ya kifurushi tulichokuwa tumeomba 😍😍," alisema chini ya video aliyochapisha Jumanne.

Alisema kuwa alipata fursa ya kuwa na wakati mzuri ambao amekuwa akitaka sana na familia yake kila wakati.

"Utukufu kwa Mungu. Nimeongeza mwaka mmoja. Familia ndiyo kwanza!" alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved