Karen Nyamu ashtumiwa kumfuata Samidoh Australia kumzuia asipate mpango wa kando, ajibu

Seneta huyo alibainisha kwamba hakuna mwanaume ambaye hutafuta mpango wa kando katika nchi ya mbali.

Muhtasari

•Shabiki alidai sababu pekee iliyomfanya mwanasiasa huyo kujiunga na Samidoh nchini Austaralia ilikuwa kulinda mipaka yake.

•“Side dish tunakuanga kanairo. Sasa ni mwanaume mgani anataka sidefish wa mbali hivyo,” Karen Nyamu alijibu.

Seneta Nyamu na mpenzi wake Samidoh
Image: FACEBOOK// KAREN NYAMU

Senetor Karen Nyamu alitoa jibu la kejeli baada ya mwanamtandao kumshutumu kwa kumfuata mpenzi wake Samidoh hadi nchini Australia ili kumzuia kutafuta mpenzi mwingine katika taifa hilo la bara Oceania.

Karen na Samidoh wamekuwa wakifurahia muda pamoja nchini Australia katika siku kadhaa za hivi majuzi. Mwimbaji huyo wa Mugithi alifanya ziara ya kikazi nchini humo mapema mwezi huu na seneta huyo wa UDA akajiunga naye huko siku chache baadaye na hata kujiunga naye kwenye matamasha yake ya muziki.

Katika moja ya machapisho yake ya Karen kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi, mtumiaji wa Instagram alidai kwamba sababu pekee iliyomfanya mwanasiasa huyo kujiunga na Samidoh nchini Austaralia ilikuwa kulinda mipaka yake.

"Alienda kuchunga bwana wa wenyewe asichukue another side chick.. Karen uko na kibarua," @dorcaskagwi aliandika chini ya post ya Instagram ya Karen.

Katika jibu lake, mama huyo wa watoto watatu alibainisha kwamba hakuna mwanaume ambaye hutafuta mpango wa kando katika nchi ya mbali.

“Side dish tunakuanga kanairo. Sasa ni mwanaume mgani anataka sidefish wa mbali hivyo,” Karen Nyamu alijibu.

Image: INSTAGRAM// KAREN NYAMU

Samidoh amekuwa akiwaburudisha mashabiki wake nchini Australia katika siku kadhaa zilizopita na mama wa watoto wake wawili amekuwa akionekana naye mara kwa mara.

Siku ya Jumatano jioni, Karen alishiriki video zao wakipelekwa na taxi kwenye nyumba moja iliyo msituni ambako walilala. Katika video hizo, wawili hao walionekana wakiburudika pamoja na hata kutaniana mara kwa mara walipokuwa wakienda nyumbani.

Kulikuwa na tukio la kusisimua ambapo seneta huyo wa kuteuliwa alimuuliza Samidoh kama anaweza kujisaidia haja ndogo nje msituni.

“Babe naweza kukokojoa hapa? Karen alimuuliza mzazi mwenzake.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za Mugithi hata hivyo kwa utani alimzuia mpenzi huyo wake dhidi ya kufanya hivyo.