Kutana na mrembo Tanasha Donna akiwa mtoto (+picha)

Tanasha alionyesha kumbukumbu kadhaa za siku zake za utotoni.

Muhtasari

•Mzazi mwenza huyo wa Diamond alichapisha picha tatu ambazo  zilipigwa katika hatua tofauti za utoto wake.

•"Mtoto T mnene akiwa Uingereza🙈" Aliandika.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Siku ya Jumatatu mwanamuziki wa Kenya Tanasha Donna alionyesha kumbukumbu kadhaa za siku zake za utotoni.

Katika ukurasa wake wa Instagram, mzazi mwenza huyo wa Diamond alichapisha picha tatu ambazo  zilipigwa katika hatua tofauti za utoto wake. Kwa kuzingatia mwonekano wake kwenye picha hizo, zote zinaonekana kupigwa alipokuwa na umri wa chini ya miaka 10.

Katika picha moja, kijana Tanasha Donna mdogo alikuwa ameshikiliwa na mama yake ambaye alikuwa pamoja na bibi mwingine. Wote walionekana wenye raha.

"🥰💕🌸" aliandika kando ya picha hiyo.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Pia alichapisha picha nyingine iliyomuonyesha akicheza pekee yake huku akiwa amekalia nyasi. Alionekana mnene kiasi kwenye picha hiyo. 

"Mtoto T mnene akiwa Uingereza🙈" Aliandika.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Mapema mwaka huu Tanasha alitembelea mama yake nchini Ubelgiji ambako huwa anapenda kutembelea mara kwa mara na kubarizi na mama yake.   Alionekana makini sana katika picha hiyo ambayo huenda  ilipigwa alipokuwa katika Shule ya Msingi.

"Lol" aliandika.

Image: INSTAGRAM// TANASHA DONNA

Mapema mwaka huu, mpenzi huyo wa zamani wa Diamond alifunguka ukweli kuhusu asili yake halisi. Alieleza kuhusu mizizi yake wakati alipokuwa ametembelea mama yake nchini Ubelgiji mwezi Agosti.

"Nilizaliwa Uingereza, nilikulia Kenya, kisha nikaondoka kwenda Ubelgiji, lakini baba wangu wa kibiolojia ni Muitaliano na mchanganyiko mwingine huko pia lakini alikua na baba wa kambo wa Ubelgiji, kisha nilirudi Kenya kama miaka 6/7 iliyopita. Huwa naenda na kurudi Ulaya/Kenya nitakapoweza" Alisema.

Mamake Tanasha, Bi Diana Oketch ni Mkenya kutoka jamii ya Luo ilhali baba yake ni mzaliwa wa Italia.