Mahaba yanoga baina ya Jux na mpenziwe anayefanana na aliyekuwa mkewe Vanessa Mdee (+picha)

Jux alimchezea Karen wimbo wa mapenzi alioufanya yeye na Mbosso 'Sing for you.'

Muhtasari

•Jux alifunga safari ya kwenda  Ufaransa siku chache zilizopita na alikuwa pamoja na mpenzi wake Karen Bujulu.

•Aliambatanisha video hiyo na wimbo wake wa mapenzi ambao alimshirikisha Mbosso 'Sing For You' kipande kinachosema,"

Jux na mpenzi wake Karen Bujulu
Image: INSTAGRAM// JUMA JUX

Staa wa Bongo RnB Juma Jux kwa sasa Jux yupo jijini Paris, nchini Ufaransa.

Jux alifunga safari ya kwenda katika nchi hiyo ya Ulaya siku chache zilizopita na alikuwa pamoja na anayedaiwa kuwa mpenzi wake Karen Bujulu.

Karen ambaye kimaumbile anafanana sana na aliyekuwa mke wa Jux, mwimbaji Vanessa Mdee ameonekana mara nyingi na mwanamuziki huyo.

Katika siku mbili zilizopita, mmiliki huyo wa duka la nguo la African Boy amekuwa akichapisha picha na video zake akifurahia muda na Karen katika jiji la Paris huku wawili hao wakionekana kutembelea maeneo mbalimbali ya burudani.

"Ilikuwa heshima kupata chakula cha jioni katika Chateau de Bagnolet .. Henessy Family House," Jux aliandika chini ya video inayomuonyesha akibarizi na mpenzi wake katika mgahawa mmoja jijini Paris.

Aliambatanisha video hiyo na wimbo wake wa mapenzi ambao alimshirikisha Mbosso 'Sing For You' kipande kinachosema,"

"Mpenzi mpenzi na leo nataka tena

Mpenzi nipe mapenzi nilale huku nasema

Ibilisi laana, laana tusimkaribishe

Tusije gombana, gombana tumfaidishe

Chumbani kwangu nimejaza picha zako,

Na kila wimbo nalitaja jina lako,

Ukiwa mbali lalimiss penzi lako,

Na nitachora tattoo niandike sifa zako babby," 

Mwimbaji huyo pia alichapisha picha na video zingine kadhaa zinazomuonyesha akiwa na Karen wakifuatilia mechi ya mpira wa vikapu kati ya Chicago Bulls na Detroit Prisons.

Pamoja nao katika uwanja huo wa mpira wa vikapu alikuwa msanii wa nyimbo za kufoka wa Kenya Henry Ohanga almaarufu Octopizzo.

Jux na Karen wakidaiwa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi mwaka jana. Mwimbaji huyo pia alimshirikisha Karen kwenye wimbo wake kama vixen.

Siku chache zilizopita, Jux alionyesha nyakati za kimapenzi na mrembo huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Kwa upande wake Karen alichapisha picha ya ndege na kuandika , "Wakati huu ninashika hisia na safari za ndege."

Wawili hao walikuwa wanaelekea Paris, mahali Jux anapenda kuenda likizo. Hata mashabiki wao walifurahi kwamba wawili hao wamerudi pamoja.