Mamake Yesu, Maria Mtakatifu anadaiwa kutokea mbele ya waumini wa kanisa moja la Katokiliki katika eneo ya Kasarani, Nairobi.
Video iliyofikia Radio Jambo inayodaiwa kuwa ya tukio hilo inaonyesha sura ya mwanamke ikiwa imemulikwa kwenye ukuta wa mbele ya Kanisa la Parokia ya St Clare. Viongozi wa kanisa na waumini waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya ibada hiyo wanasikika wakipiga kelele na kusifu wakati picha hiyo ikioonyeshwa.
Baadhi ya waumini walionekana wakirekodi tukio hilo huku wengine wakiinua mikono na kusema sala na kumsifu Mungu.
Tazama video hapa:-
Haijabainika kama kweli tukio hilo lilitokea au ilikuwa ni ukarabati wa teknolojia lakini Wakenya wameendelea kwa maoni mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, wengi wao wakionekana kulitupilia mbali.
Soma maoni ya baadhi ya wanamitandao Wakenya;
nimrodnick: ๐๐๐๐๐๐na unaniambia cocaine ndio dawa mbaya zaidi
christinewawira: Ikiwa mababu zetu wangeweza kuona kile ambacho tumekuwa sasa ๐
brasho: Tunajua mwangaza wa projekta, watu sio wajinga buana
backyard_thriftplug: Sitaki kucomment vibaya nikose kuenda heaven ju ya comment tu๐
misskithinji Mwenye aliambia watu Bikira Maria anakaa hivo ni nani?
boazinhoke utANASWAA EEEEEH๐๐๐, the pastors wameshangaa kutushinda sisi wenye tuko nyumbani
ericnjiru: Patia Mary simu
me.see Hata nimevaa miwani na bado hakuna kitu naona