Mchekeshaji Elsa Majimbo amtambulisha mpenzi wake mzungu (+picha)

Majimbo alichapisha picha na video za baadhi ya nyakati zao wakiwa pamoja.

Muhtasari

•Majimbo ,21, alimtambulisha mpenziwe hadharani kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi jioni kupitia Instagram.

•Mpenzi wa Majimbo ni mcheza santuri na mtayarishaji ambaye anajitambulisha kama Dj Hakeem.

Image: INSTAGRAM// ELSA MAJIMBO

Mchekeshaji maarufu wa Kenya Elsa Majimbo hatimaye amemtambulisha mwanaume ambaye anachumbiana naye.

 ambapo alichapisha picha na video za baadhi ya nyakati zao wakiwa pamoja.

"Kwa mpenzi wangu, asante kwa kuniletea furaha nyingi, upendo, furaha," Majimbo aliandika chini ya picha hizo.

Alitumia nafasi hiyo kumshukuru mpenzi wake kwa kumbukumbu walizotengeneza pamoja na kumfundisha  mahaba.

Katika picha na video tofauti alizopakia, wawili hao walionekana wakiwa na furaha pamoja na wenye kupendana sana.

Kwa kuzingatia mwonekano katika picha na video hizo, mwanaume ambaye mchekeshaji huyo alimtambulisha kama mpenzi wake ni mweupe, amemzidi umri kwa miaka kadhaa na ana ndevu kubwa usoni.

Utafiti wa haraka kwenye mitandao ya kijamii ulibainisha kuwa mpenzi wa Majimbo ni mcheza santuri na mtayarishaji ambaye anajitambulisha kama Dj Hakeem na kuna ushahidi wa mapenzi yao kwenye ukurasa wake wa Instagram. Mchekeshaji huyo Mkenya amekuwa akiandika jumbe za kimahaba chini ya machapisho mengi ya mcheza santuri huyo kwenye Instagram, uthibitisho kwamba wamekuwa pamoja kwa muda.

Haya baadhi ya maoni ya wanamitandao:

@burgerrock Upendo ni kweli! Nimefurahi sana kwa ajili yako amiga.

@leomieanderson Sawa ninyi nyote ni mnapendeza au vipi

@noordinarynoire Nimeipenda sana hii rafiki

@gleise Wow ako kwenye mapenzi 😍😍😍 na napenda hilo rafiki yangu❤️  kwa kweli, picha ya tatu kwangu #mood 😂🤣🙌🏼🔥🔥🔥

@elainewelteroth Ninapenda hadithi hii ya mapenzi ❤️😍 siwezi kungoja kukutana naye na dada mkubwa tumuache IRL