Mfahamu mpenzi mpya wa Harmonize mwenye umbo la kupagawisha

Ili kuthibisha mapenzi yake kwa Phiona, Harmonize alidokeza kwamba anapanga kuchorwa tattoo yake.

Muhtasari

•Konde Boy alidokeza amemfahamu Phiona kwa miaka minne iliyopita akitaja kuwa ni wakati mwafaka wa kujaribu mahusiano.

•Phiona ameweza kuvutia hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana na umbo maalum wa mwili wake.

amemtambulisha Phiona kama mpenzi wake mpya.
Harmonize amemtambulisha Phiona kama mpenzi wake mpya.
Image: HISANI

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ametangaza wazi kwamba hayupo single tena.

Takriban miezi mitano baada ya kutengana na muigizaji Frida Kajala Masanja, bosi huyo wa Konde Music Worldwide amemtambulisha mrembo wa Rwanda Phiona almaarufu Yolo the Queen kama mpenzi wake mpya.

"Sawa, siko single tena nimechukuliwa tayari," mwimbaji huyo alisema kwenye ukurasa wake wa mtandao siku ya Jumatatu.

Konde Boy alidokeza amemfahamu Phiona kwa miaka minne iliyopita akitaja kuwa ni wakati mwafaka wa kujaribu mahusiano.

Huku akionekana kuwatupia vijembe wapenzi wake wa zamani k.m Kajala Masanja, Wolper na Sarah Michelloti, alibainisha kuwa mwanasosholaiti huyo wa Rwanda ni zaidi ya wanawake wote ambao aliwahi kuchumbiana nao.

"Naona ni wakati wa kukuonyesha jinsi nilivyo mwanaume wa kweli. Nakupenda sana Yolo The Queen. Umepita kila msichana niliyekutana naye maishani mwangu. Umenifanya hata nijisikie kuwa mimi ni Mnyarwanda," alisema.

Aliendelea kudokeza kwamba hata anapanga kununua nyumba nchini Rwanda ili mradi tu kuwa karibu na mpenzi wake mpya.

Ili kuthibisha mapenzi yake kwa mlimbwende huyo, staa huyo wa bongo fleva alidokeza kwamba anapanga kuchorwa tattoo yake ambayo kulingana naye, itakuwa ya mwisho kabisa kuchorwa mwili mwake.

"Sawa, napata tattoo yangu ya mwisho. Sitokuja choraga tena. Bila shaka ni ya uso wako mzuri Phiona," alisema.

Phiona anasemekana kuwa mmoja wa wanasosholaiti waliofanikiwa zaidi nchini Rwanda na viunga vyake. Ameweza kuvutia hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana na umbo maalum wa mwili wake.

Mwanadada huyo mrembo amebarikiwa kuwa na mwili uliopinda na makalio makubwa ambayo wanaume wengi wanayatamani. Anajulikana zaidi kwa misemo yake ya kuvutia 'Wake Pray Slay' na 'Tamu kuliko asali.'

Haya yanajiri takriban miezi mitano baada ya mahusiano ya Harmonize na Kajala kutamatika kwa njia isiyoeleweka. 

Hivi majuzi, Kajala alidokeza kwamba alimtema msanii huyo wa zamani wa lebo ya WCB kwa sababu ya mazoea.

"Sijui niseme nini. Labda mazoea. Mtu akishakuzoea sana anakuchukulia poa," alisema.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alidokeza kwamba Harmonize bado hakuwa tayari wakati alipoamua kutulia naye kwenye mahusiano na kuwa huenda alihitaji nafasi ya kufanya mambo yake binafsi.

"Yaani mimi hata simlaumu, kwa sababu yeye ni kijana mdogo. Labda alihitaji nafasi, tulikuwa tuko karibu sana.

Yeye mara ya kwanza nahisi labda aliona kama mzaha akisema nataka huyu mtu, nataka niwe naye 24/7.  Mnaamka wote mnaenda gym, mnafanya hiki na kile. Labda alikuwa anahitaji nafasi yake afanye vitu vyake," alisema.

Kajala alibainisha kwamba alikubali kurudaina na bosi huyo wa Konde Music Worldwide kwa kuwa bado alikuwa anampenda.