"Mimi ni baba bora uliwahi kuwa naye!" Harmonize amfokea Paula huku akifunguka alivyomlipia karo

Mwanamuziki huyo alimuonya Paula kuwa atapata laana iwapo ataendelea kumkosea heshima.

Muhtasari

•Harmonize alimfahamisha Paula ingekuwa vyema kwake asingejiingiza kwenye vita ya maneno ambayo imekuwa ikiendelea kati yake na Kajala.

•Konde Boy alijigamba kuwa baba bora kwa Paula na hivyo kumuonya kuwa atapata laana iwapo ataendelea kumkosea heshima.

amesema alimlipia karo Paula Kajala.
Harmonize amesema alimlipia karo Paula Kajala.
Image: INSTAGRAM

Staa wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amedokeza kuwa alimlipia karo ya shule binti wa muigizaji Kajala Masanja, Paula kwa muda.

Konde Boy alitoa madai hayo kwenye Instagram wakati alipokuwa akimshambulia mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 21 siku ya Alhamisi baada ya kuingilia kati vita kati yake na mamake.

Katika ujumbe wake, bosi huyo wa Konde Music Worldwide alimfahamisha Paula kuwa ingekuwa vyema kwake asingejiingiza kwenye vita ya maneno ambayo imekuwa ikiendelea kati yake na Kajala katika siku chache zilizopita.

“Wewe mtoto ungenyamaza tuu maana hapo nilikwambia uji snap na hata baiskeli aliyonunuliwa bimkubwa wako na mwanaume huwezi,” Harmonize alimwambia Paula siku ya Alhamisi.

Konde Boy alijigamba kuwa baba bora kwa mwanamitindo huyo na hivyo kumuonya kuwa atapata laana iwapo ataendelea kumkosea heshima.

 "Kwa hivyo mimi ndiye baba bora umewahi kuwa naye. Hadi alafu umuulize akuambie tumeanza kulipa adaa upo langapiii mtoto mdogo. Utapata laana nyengine!!,” alisema.

Mwimbaji huyo wa kibao ‘Single Again’ wakati huohuo alibainisha kuwa alijitahidi sana wakati akiwa kwenye mahusiano na Kajala na kudokeza kuwa sasa ni wakati wa kila mtu kuendelea na maisha yake.

Harmonize na Paula walitumia muda mwingi wa Alhamisi jioni kushambuliana kwa maneno kwenye mtandao wa Instagram. Vita iling’oa nanga baada ya bosi huyo wa Konde Music Wordwide kumshambulia mpenzi wake wa zamani Kajala Masanja na kuibua shutuma kadhaa dhidi yake na bintiye.

Mapema siku ya Alhamisi, Konde Boy alidai kuwa binti huyo wa Kajala Masanja hamchukii bali alipatwa na wivu tu.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide alidai kuwa mwanamitindo huyo alimtafuta hata kabla hajaanza kutoka kimapenzi na mama yake Kajala.

Konde Boy alidai kuwa mrembo huyo mwenye umri wa miaka 20 alimtafuta kupitia kaka yake wa kambo akiwa na matumaini ya kuwa na uhusiano wa karibu naye.

“Ki ukweli kabisa hanichukii (Paula). 2017 alinitafuta kupitia mdogo wake wa kiume POL wa baba mmoja. Aliniambia dada yangu anataka kuongea nawe, huu ndio ukurasa wake wa Instagram. Nikusaidie tum binti yupo Instagram tangu 2017, mimi na machizi wenzangu tunajua!! Wee unajua kaanza mwaka juzi,” alisema Harmonize wakati akimjibu aliyekuwa mpenzi wake, Kajala Masanja.

Aliongeza, "”Niliongea naye na akanipa namba yake, na akasema usimuambie mama nyingi sana. Sikumzingatia pia alikuwa mtoto sana na ukiizingatia alikuwa shule bado. Baada ya miaka miwili anakuta penzi limekolea, nakujali, nakuhudumia, kila unachotaka nakupatia na hata yeye pia nampa atakacho kama binti yangu akaanza kuumua nini hivi!! Alitamani awe yeye, alianza kuomba pesa zaidi."

Konde Boy alisema licha ya yote aliendelea kumheshimu mwanamitindo huyo hadi alipogundua kuwa ex wake, Kajala alikuwa akitumia simu yake kuzungumza na wanaume wengine.

Pia alidokeza kuwa alishangaa sana baada ya madai kuwa alikuwa akijaribu kumtongoza Paula kuibuka na kudai kuwa hapo awali walikuwa wamewahi kushiriki mazungumzo kama hayo mara nyingi bila shida yoyote.

“Baada ya kugundua nyinyi ni marafiki tu mnanichora ikabidi nianze kumjibu kwa nguvu zoteee. Kwa hiyo hata suala la zima taaa nashangaa tu siku ile ilikuwaje ikiwa tulishaingea mara kibao tuu maongezi ya namna ile,” alisema.

Katika majibu yake, Paula alimtaka mwanamuziki huyo kumuacha na kumwangazia mwanamke anayedaiwa kupata naye mtoto.

“Hii namba usiiguse kabisa!!! Sitaki kukuvunjia heshima. Siko kwenye mood kabisa leo. Achana na mimi. Achana na mimi. Kama wewe unavuta b*ngi mdomo mimi navuta m*tak*ni. Sasa tulia,” Paula alijibu.