logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtoto wa 3? Kabi adokeza kuwa mkewe Milly Wajesus ni mjamzito

Wanamitandao waliwapongeza wawili hao kufuatia chapisho hilo.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri09 January 2023 - 20:42

Muhtasari


•Kabi alidokeza kuhusu mtoto mwingine siku ya Jumatatu jioni baada ya kuchapisha picha ya mkewe Milly akiwa mjamzito.

•Takriban miezi miwili baada ya kujifungua, Milly Wajesus alidokeza kuhusu mpango wa kupata mtoto wa tatu.

Wanandoa mashuhuri Peter Kabi na Millicent Wambui wa The Wajesus Family huenda wanatarajia mtoto wao wa tatu pamoja.

Kabi alidokeza kuhusu mtoto mwingine siku ya Jumatatu jioni baada ya kuchapisha picha ya mkewe Milly akiwa mjamzito kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha picha hiyo na ujumbe wa kimafumbo akidokeza kwamba mama huyo wa watoto wawili anabeba ujauzito mwingine, chini ya mwaka mmoja baada ya kumkaribisha mtoto wao wa pili pamoja.

"Asante Mungu kwa matunda ya tumbo,na kuombea leo wacha mipango yako ikazae matunda katika jina la Yesu,"Kabi Aliandika.

Wanamitandao waliwapongeza wawili hao na hizi hapa baadhi ya jumbe zao;

deborah_mercyful: I knew she was pregnant wow congratulations

debra_omwenga: Amen... And praises yo the lord❤️❤️

aliyah__khxn_: Inserts DJ Khaled's voice: Another one 😄. Congratulations 👏✨

wambui_wa_naivasha: May God bless every Waiting Womb❤️. Mum of Angel's, Pregnant mum's and all mum's in general🙏❤️

nazshizzIndeed:  in Gods times He makes thing beautiful #Ni Jesus all the way

miss_munywoki: Wueeeeh enyewe mapema ndio best, all the best the kabis

Mwezi Aprili, mwaka uliopita wanavlogu hao wawili walibarikiwa na mtoto wa kike, ambaye walimtambulisha mitandaoni hivi juzi.

Takriban miezi miwili baada ya kujifungua, Milly Wajesus alidokeza kuhusu mpango wa kupata mtoto wa tatu.

Mama huyo wa watoto wawili hata hivyo alibainisha kuwa angechukua muda kabla ya kuongeza mtoto mwingine. 

"Ninapenda watoto wachanga na familia kubwa, kwa kweli sijamaliza kuzaa lakini sasa ninahitaji wakati wa kujipanga," alisema kwenye Instagram wakati akimjibu shabiki ambaye aliuliza ikiwa anafikiria kuwa na watoto zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved