Mtoto wa Kistaa! Paula Kajala na Marioo wafichua wanatarajia mtoto wa kwanza pamoja

Mastaa wa Bongo Marioo na Paula Kajala watakuwa wazazi hivi karibuni.

Muhtasari

•Wawili hao wametoa tangazo la kipekee la pamoja wakifichua kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

•Paula alionekana na ujauzito mkubwa huku yeye na mpenzi wake wakionyesha picha za kijusi kinachokua tumboni mwake.

Image: INSTAGRAM// MARIOO

Mastaa wa Bongo Marioo na Paula Kajala watakuwa wazazi hivi karibuni.

Wapenzi hao maarufu mnamo Alhamisi asubuhi walitoa tangazo la kipekee la pamoja wakifichua kwamba wanatarajia mtoto wao wa kwanza pamoja.

Wawili hao walishiriki video nzuri iliyowaonyesha wakisoma gazeti lenye kichwa cha habari cha ‘A baby is on the way’ na pia kuonyesha tumbo la Paula lililochomoza.

“Ninatarajia mtoto na mpenzi wangu. Kuanzia mbili hadi tatu,” Paula aliandika chini ya video ambayo alichapisha kwenye Instagram.

Katika video hiyo, mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 22 alionekana akiwa na ujauzito mkubwa huku yeye na mpenzi wake wakionyesha picha za kijusi kinachokua tumboni mwake.

Marioo ambaye kwa jina halisi ni Omary Mwanga pia alishiriki furaha yake ya kuwa baba hivi karibuni na akamshukuru binti wa muigizaji Kajala Masaja kwa kubeba ujauzito wake.

"Kuongeza mwanachama mpya kwenye kikosi chetu! Soon inshallah.. Najivunia wewe malkia @therealpaulahkajala Mungu akubariki wewe na familia,” Marioo alisema.

Mapema mwaka huu, muigizaji Fridah Kajala Masanja alithibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba hivi karibuni ataitwa bibi [nyanya] shukrani kwa juhudi za haraka za bintiye wa kipekee, Paula Kajala.

Kajala alionyesha furaha akifichua taarifa hizo ila akaonesha hisia kwamba bintiye aliharakisha kwani yeye [Kajala] hakuwa tayari kuanza kuitwa nyanya kwani bado anajiona mbichi licha ya umri wake kusonga kwa kasi ya ajabu.

“Ila Paula muda wa kuwa bibi ulikuwa bado kidogo jamani,” Kajala aliandika akiwa katika picha nzuri kwenye ufuo wa bahari.

Kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja sasa, Paula na msanii Marioo wamekuwa katika kile kinachotajwa kuwa mapenzi mazito, huku Kajala mwenyewe akiliafiki penzi lao na kumtaja waziwazi Marioo kama mkaza mwana wake.

Mwaka jana, Paula na mamake Kajala walithibitisha kwamba Marioo alikuwa amewasilisha mahari za zaidi ya milioni 100 za kitanzania kwa ajili ya kumuoa kabisa mrembo huyo ambaye pia ni mjasiriamali wa mavazi.

“Tayari ametoa mahari milioni 100,” Paula alijibu swali hilo huku wakicheka na mama yake na kujaribu kuficha nyuso.

Licha ya udogo wa umri wake, binti huyo amekuwa katika mzunguko wa kimapenzi hapo awali na msanii Rayvanny ambaye mapema mwaka jana waliachana bosi huyo wa NLM kumrudia mpenzi wake wa zamani, Fahyma.