"Mtoto wa ujana wangu!" Samidoh aungana na Edday Nderitu kusherehekea mtoto wao wa kwanza (+picha)

Msanii huyo alimtambua bintiye kama mtoto wa ujana wake na alifunguka kuhusu hali iliyozingira kuzaliwa kwake.

Muhtasari

•Shirleen ambaye ni mtoto wa Samidoh na mke wake wa kwanza Edday Nderitu hivi majuzi alihitimu kuenda shule ya upili na wazazi wote wawili walikuwepo kumsherehekea. 

•Samidoh aliendelea kusherehekea ukuaji wa binti yake na kuzungumza kuhusu jinsi anajivunia ukuaji wake.

Samidoh, Shirleen, na Edday Nderitu
Image: INSTAGRAM// SAMIDOH

Staa wa Mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh amemsherehekea binti yake mzaliwa wa kwanza Shirleen Muchoki kufuatia mafanikio makubwa.

Shirleen ambaye ni mtoto wa mwanamuziki huyo na mke wake wa kwanza Edday Nderitu hivi majuzi alihitimu kuenda shule ya upili na wazazi wote wawili walikuwepo kumsherehekea. Pia ameadhimisha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Huku akimsherehekea siku ya Jumamosi, mwimbaji huyo alimtambua bintiye kama mtoto wa ujana wake na alifunguka kuhusu hali iliyozingira kuzaliwa kwake.

Alizungumza kuhusu jinsi Shirleen alizaliwa katika siku zake za mapema za ujana na jinsi hakujua la kufanya alipozaliwa.

“Binti yangu, mtoto wa ujana wangu, ulizaliwa muda mfupi baada ya kutoka katika ujana wangu. Ilikuwa ni wakati wa kutatanisha sana kwangu. Sikujua kama nirudi shuleni, nikushughulikie, au nijitegemee,” Samidoh aliandika kwenye Instagram.

Mwanamuziki huyo mahiri aliambatanisha ujumbe wake na picha zilizomuonyesha yeye, bintiye, mzazi mwenzake Edday Nderitu na watoto wao wengine.

Samidoh aliendelea kusherehekea ukuaji wa binti yake na kuzungumza kuhusu jinsi anajivunia ukuaji wake. Pia alimpongeza kwa ufaulu wake wa kuhitimu elimu ya upili.

"Yetu imekuwa safari ambayo tumeona kila mmoja akikua. Leo, ninajivunia sana. Ninavyoona unahitimu kuingia shule ya upili - hii! Nisingeikosa kwa lolote  duniani. Msichana wangu, nakutakia ukuu. Nenda ukashinde kwa sababu ulimwengu ni wako. Hongera!!,” aliandika.

Mwimbaji huyo aliongeza, "Unapofikisha mwaka mmoja zaidi, ninakutakia Siku njema ya Kuzaliwa. Asante kwa kumfanya Baba awe na kiburi.

Samidoh amekuwa Marekani katika siku za hivi majuzi ambapo amekuwa akitumia muda mzuri na familia yake inayoishi huko.

Mke wa msanii huyo wa miaka mingi, Edday Nderitu kwa sasa anaishi Marekani pamoja na watoto wao.  Aliondoka nchini mapema mwaka jana na anaonekana tayari kutulia huko vizuri huku watoto wakiwa wameanza shule huko.

Mwezi Julai mwaka jana, Bi Edday Nderitu aliweka wazi kwamba alimuacha mumewe ili awe na mwanamke ambaye alionekana kumtaka zaidi.

"Wacha nifafanue mambo machache ambayo yalishirikiwa mtandaoni na sio sahihi. Siko kwenye ndoa ya wake wengi, kama ilivyoelezwa nilimuacha mume kwa yeyote aliyemhitaji zaidi,” Edday alisema kupitia Facebook.

Aliongeza, "Nilifanya uamuzi wa kujiondoa mimi na watoto wangu kutoka kwa mazingira hayo yenye sumu, haswa binti yangu kijana ambaye kwa bahati mbaya anapokea moja kwa moja tabia isiyoaminika iliyoonyeshwa."