logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mumewe Zari, Shakib afichua wanaume wenzake wanaumezea mate mwili wake na kumtumia meseji

Shakib alieleza kuwa wanaume wenzake wengi wamekuwa wakimtumia jumbe wakimsifia kuhusu jinsi mwili wake ulivyo mzuri.

image
na Radio Jambo

Makala06 July 2023 - 04:54

Muhtasari


•Shakib Cham Lutaaya amefichua kwamba kuna wanaume wengi ambao wamekuwa wakiumezea mate mwili wake.

•"Amka tu, jipe ​​muda, nenda kafanye mazoezi, kula na basi utapata kitu kama changu au bora kuliko changu. Ni rahisi hivyo,” Shakib alisema.

Mume wa mwanaosholaiti na mfanyibiasara mashuhuri wa Uganda Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amefichua kwamba kuna wanaume wengi ambao wamekuwa wakiumezea mate mwili wake.

Akizungumza kwenye video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatano, Mganda huyo mwenye umri wa miaka 31 alieleza kuwa wanaume wenzake wengi wamekuwa wakimtumia jumbe za kumpongeza na kumsifia kuhusu jinsi mwili wake ulivyo mzuri.

"Mara nyingi huwa napata meseji nyingi kutoka kwa wanaume wenzangu wengi wakiniambia nina mwili sawa, nina mwili mzuri," Shakib alisema.

Aliendelea, "Pia nyie hamjachelewa, mnaweza kuwa na mwili kama wangu au mnaweza kuwa na kitu bora zaidi kuliko nilicho nacho."

Mfanyibiashara huyo aliendelea kuwashauri wanaume ambao wamekuwa wakivutiwa na mwili wake kufanya mazoezi na kula vizuri ili kupata mwili mzuri kama wake.

"Amka tu, jipe ​​muda, nenda kafanye mazoezi, kula na basi utapata kitu kama changu au bora kuliko changu. Ni rahisi hivyo,” alisema.

Shakib, 31, alikuja kujulikana zaidi baada ya mahusiano yake na mpenzi wa zamani wa Diamond Zari Hassan, 42, kufichuka hadharani mapema mwaka jana. Wawili hao walikuwa wamefahamiana kwa miaka kadhaa kabla ya kujitosa kwenye mahusiano ya kimapenzi ambayo yamefikia hatua ya ndoa tayari.

Wawili hao walifunga ndoa ya Kiislamu almaarufu Nikkah mwezi uliopita baada ya kuchumbiana kwa takribani mwaka mmoja. Walivishana pete katika hafla ya faraghani ambayo ilihudhuriwa na idadi ndogo ya watu wakiwemo wanafamilia na marafiki.

Katika picha na video za hafla hiyo iliyofanyika chumbani ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, wapenzi hao walionekana wamevalia Kiislamu kabisa huku wote wakiwa wameketi kwenye mkeka uliotandikwa sakafuni.

Shakib alionekana akiinama kwa goti moja na kumvisha Zari pete ya ndoa kwa furaha kabla ya wawili hao kupigana mabusu huku watu wachache waliohudhuria hafla hiyo wakiwasherehekea kwa makofi.

Sio mengi ambayo yanayojulikana hadharani kumhusu Shakib kabla ya mahusiano yake na Zari Hassan. Kabla ya kuchumbiana na Shakib, Zari aliwahi kuwa kwenye ndoa na marehemu Ivan Ssemwanga kisha akachumbiana na staa wa bongo Diamond Platnumz na mfanyibiashara wa Uganda GK Choppa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved