"Namkatalia!" Paula akataa ndoa baada ya Rayvanny kumuonyesha mahaba mazito

Awali Rayvanny alidokeza kuwa bado angali na hisia za mapenzi kwake.

Muhtasari

•Paula alidokeza kwamba mtu ambaye ana nia ya kumuoa sasa anataka tu kumharibia maisha yake.

•Rayvanny alichapisha picha ya Paula na kuambatanisha na emoji za moyo, ambazo kawaida hutumika kuashiria mapenzi.

Rayvanny ajuta kumpenda Paula
Rayvanny ajuta kumpenda Paula
Image: Maktaba

Mwanamitindo mashuhuri  wa Tanzania, Paula Paul Kajala amedokeza kwamba hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni.

Katika chapisho lake la hivi punde kwenye mtandao wa Tiktok, Paula aliiga sauti ya mwanamke akiweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa.

"Mwanaume akisema anataka kukuoa sasa hivi utamchukulia aje?" sauti ya mwanaume iliuliza kwenye video.

Sauti ya mwanamke ilijibu huku ilisema kwamba mtu ambaye ana nia ya kumuoa sasa anataka tu kumharibia maisha yake.

"Sitamchukulia vibaya. Si namkatalia tu. Anayetaka kunioa, anataka kuniharibia maisha," 

Chapisho la kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 lilikuja masaa machache tu baada ya staa wa Bongofleva Raymond Mwakyusa almaarufu Rayvanny kudokeza kuwa bado angali na hisia za mapenzi kwake.

Usiku wa kuamkia Jumapili, Rayvanny alichapisha picha ya binti huyo wa muigizaji  Frida Kajala Masanja na chini yake kuambatanisha na emoji za moyo wenye moto, ambazo kwa kawaida hutumika kuashiria mapenzi.

"❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥❤️‍🔥,"  aliandika kwenye picha nzuri ya kipusa huyo mwenye umri wa miaka 20 ambayo alipakia Instagram.

Hatua hiyo ilidokeza kuwa huenda wawili hao bado wana uhusiano mzuri licha ya kudaiwa kuachana zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Baadhi walichukulia kitendo cha Rayvanny kama dokezo kuwa wamerudiana.

Hayo yalitokea takriban mwezi mmoja baada ya msanii huyo wa zamani wa WCB kudokeza kuwa anajuta kutengana na Paula.

Mwezi uliopita, bosi huyo wa Next Level Music alichapisha picha ya kumbukumbu ya siku zake na Paula kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Rayvanny aliambatanisha picha hiyo yake na binti huyo wa muigizaji mkongwe Kajala Masanja wakiwa wameketi kwenye kiti na emoji ya uso uliofunikwa kwa kiganja cha mkono ambayo mara nyingi huashiria  kufadhaika au aibu.

Ingawa hakushiriki maelezo zaidi, emoji hiyo pengine ilikusudiwa kufupisha hisia zake za jumla kuhusu uhusiano wao uliovunjika.

Mwaka jana wakati akitumbuiza katika tamasha la Fiesta 2022 mjini Sumbawanga, Tanzania, Rayvanny alidokeza kusambaratika kwa mahusiano yake ya muda mrefu na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 20.

Alidokeza hayo wakati akitumbuiza wimbo wake 'Naogopa' ambapo aliongeza mistari kadhaa iliyosikika kama ujumbe wa kukiri.

"Mapenzi yasikuchanganye nakwambia, usije ukapata bila kama Dulla. Mapenzi usije kufananisha,  kama  vile chakula. Nilinyosha moyo Karula, nikaachana na Paula..." aliimba.

Baadaye, mwandani huyo wa Diamond Platnumz alidaiwa kuzozana na Paula, madai ambayo alipuuzilia mwishoni mwa mwezi Oktoba.