"Nina haki ya kufanya chochote!" Nandy afunguka kuhusu kusoma meseji za mumewe Billnass

Muhtasari

•Nandy alisema mpenzi wake yupo huru kuchukua simu yake na vilevile mumewe hajawahi kumzuia yeye kuchukua simu yake.

•Mapema mwaka huu, rapa Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba baada yake kukubali ndoa naye.

Billnass na Nandy
Billnass na Nandy
Image: Nandy (Facebook)

Mwanamuziki wa Bongo Faustina Mfinanga almaarufu kama Nandy amefichua kwamba yeye na mpenzi wake Bill Nass hubadilishana simu wakati wowote.

Akihutubia waandishi wa habari katika hafla ya kuzindua Funguka Campaign, Nandy alisema mpenzi wake yupo huru kuchukua simu yake na vilevile mumewe hajawahi kumzuia yeye kuchukua simu yake.

"Ni kama tunatumia simu zetu pamoja. Simu yake naweza nikachukua muda wowote, simu yangu anaweza akachukua muda wowote. Sidhani kama atakuwa anachukua aende kusoma jumbe  moja kwa moja. Ana haki ya kufanya chochote, pia mimi nina haki ya kufanya chochote kwenye simu yake," Nandy alisema.

Malkia huyo wa muziki alikiri kwamba huwa anapitia jumbe zilizo kwenye simu ya mumewe. Hata hivyo alisisitiza kwamba hana shaka naye na anamwamini sana.

"Siwangi rasmi eti nataka kusoma kwa sababu nina shaka naye, hapana. Namwamini!" Alisema.

Mapema mwaka huu, rapa Billnass alimvisha Nandy pete ya uchumba baada yake kukubali ndoa naye. 

Billnass aliposa kwa mpenzi huyo wake mwezi Februari na kwa mara ya pili Nandy akakubali kufunga pingu za maisha naye.