logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nataka hili milele" Shakib aonyesha upendo kwa wanawe Zari huku kukiwa na uvumi wameachana

Shakib amedokeza kuwa bado ana uhusiano mkubwa na familia ya mke huyo wa zamani wa Diamond.

image
na Radio Jambo

Makala31 January 2023 - 06:26

Muhtasari


•Zari aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake na Shakib baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

•Shakib amedokeza kuwa bado ana uhusiano mkubwa na familia ya mke huyo wa zamani wa Diamond Platnumz.

Shakib Cham Lutaaya amedokeza kwamba mahusiano yake na mwanasoshalaiti Zari Hassan bado yapo imara huku kukiwa na tetesi za kutengana.

Hivi majuzi, Zari aliibua wasiwasi kuhusu mahusiano yake na kijana huyo Mganda mwenye umri wa miaka 31 baada ya kuchapisha nukuu ambayo ilielezea hatari ya uwongo miongoni mwa watu wako wa karibu.

Baadhi ya watu hawaelewi jinsi uwongo unaweza kuwa sumu. Uongo huambukiza na kulaani mahusiano yenye furaha hadi unahisi kuumwa na tumbo kwa kuwaamini tena,

Haijalishi ni kiasi gani unampenda mtu, wakati mwingine huwezi kujizuia kujisikia kama aliiba Faraja yako. Huna raha tena kwa sababu unakisia kila kitu. Sasa, kuwaamini sio kazi rahisi. Sasa inahitaji bidii na wakati mwingine hiyo inachosha ilisomeka nukuu hiyo ya Horacio Jones ambayo alichapisha kwenye Snapchat.

Nukuu hiyo na muda ambao alichapisha vilionekana kuwaacha wanamitandao na maoni tofauti huku wengi wakikisia kwamba ni ishara wazi kuwa yote sio sawa ndani ya mahusiano yake ya miezi kadhaa na Shakib.

Hata hivyo, Shakib sasa amedokeza kuwa bado ana uhusiano mkubwa na familia ya mke huyo wa zamani wa Diamond Platnumz.

Jumatatu, Mganda huyo anayeshi Afrika Kusini alichapisha picha ya watoto  wa Zari; Pinto Tale, Tiffah Dangote na Prince Nillan na kuwaonyesha upendo watatu hao. Aliambatanisha chapisho hilo na wimbo wa Drake, Forever, kipande kinachosema, "It may not mean nothing to y'all, Understand nothin' was done for me, So I don't plan on stoppin' at all, I want this sh*t forever man, ever man, ever man I'm sellin' sh*t down at the mall

Inatafsiriwa: (Inawezekana isimaanishe chochote kwenu, Lakini elewa kwamba hakuna nilichofanyiwa, kwa hivyo sina mpango wa kuacha kabisa, nataka hili milele, milele. Nauza hili chini kwenye maduka

Pia aliambatanisha ujumbe huo na emoji ya moyo ambayo mara nyingi huashiria upendo.

Zari na Shakib wamekuwa katika mahusiano yaliyokosolewa sana kwa miezi kadhaa sasa huku mwanasoshalaiti huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 41 tayari akitoa dokezo la kutaka kutulia na mpenzi huyo wake mwenye umri wa miaka 31.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved