"Nimekubali nimekaliwa, niliolewa!" Bahati akiri, afichua Diana Marua huingia nyumbani baada yake

Bahati alikiri kwa utani kuwa Diana ndiye aliyemuoa.

Muhtasari

•Mwimbaji Kelvin  Bahati amekiri kwamba amekubali amekubali kutawaliwa na mke wake, Diana Marua.

•Bahati alifichua kuwa hivi majuzi mkewe amekuwa akifika nyumbani jioni sana baada yake, jambo ambalo hana shida nalo.

Diana Marua na mume wake Bahati
Image: INSTAGRAM// BAHATI

Mwimbaji mashuhuri Kelvin Kioko almaarufu Bahati amekiri kwamba amekubali amekubali kutawaliwa na mke wake, Diana Marua.

Akizungumza kwenye ukurasa wake wa Instagram siku ya Jumatatu, Bahati alikiri kwa utani kuwa Diana ndiye aliyemuoa.

Aidha, baba huyo wa watoto watano alibainisha kuwa kukubali kutawaliwa na mke ni jambo nzuri kwa mwanaume.

"Nimekubali, nimekaliwa. Siri ni kukubali kukaliwa," alisema.

Bahati alifichua kuwa hivi majuzi mkewe amekuwa akifika nyumbani jioni sana baada yake, jambo ambalo hana shida nalo.

"Nilikuwa nimelala alafu bibi akarudi. Siku hizi bibi yangu anaingia baada yangu. Niliolewa. Saa hii ameniamsha nikule," alisema chini ya video yake na Diana Marua wakipata chakula chao cha jioni pamoja.

Diana aliweka wazi kwamba alikuwa ametoka kwenye chumba cha mazoezi kabla ya kuingia jikoni kumpikia mumewe.

Bahati ambaye alionekana wazi kufurahia chakula hicho alibainisha kuwa kila siku anataka kula vyakula vilivyopikwa na mkewe.

"Kama hivi ndio napikiwa na mke wangu, nisiwahi kuona Irene amenipikia chakula. Akae na hizo chemsha zake," alisema.

Bahati na Diana wamekuwa pamoja kwa zaidi ya nusu muongo na wamejaliwa watoto watatu pamoja. Ndoa yao ni mojawapo ya miungano inayokosolewa zaidi nchini Kenya ikizingatiwa kuwa Diana ni mzee kuliko mwimbaji huyo.

Mapema mwezi jana, Diana alisherehekea miaka saba ya kuwa pamoja na mwimbaji huyo wa zamani wa nyimbo za injili.

Katika chapisho la Instagram, mama huyo wa watoto watatu alionyesha fahari yake kuona jinsi wanavyofanana sana.

Alibainisha kuwa yeye na Bahati wanafanana sio kimuonekano tu bali pia, kimavazi na hata lugha yao ni sawa.

"Miaka 7 ambayo imepita, tunafanana 😂, tunaongea lugha moja, vicheko vyetu ni vinafanana na tangu wakati wote hatujawahi kuacha kufananisha mavazi yetu 💃," aliandika chini ya picha zake na mumewe wakiwa na mavazi sawa.

Mwanavlogu huyo wa YouTube alidokeza kuwa mapenzi yake na mwanamuziki huyo mahiri ni ya kweli na ya kujivunia.

Bahati kwa upande wake alibainisha kuwa maisha yake yalikamilika wakati ambapo alimpata mke huyo wake na kuweka wazi kuwa amemtosha.

"Nilipokupata, nilipata nusu yangu bora na unatosha Diana Marua," alisema kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Bahati alimtambulisha Diana kama 'mshirika wake wa maombi' takriban miaka sita iliyopita kabla ya kubainika kuwa wanachumbiana.

Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja katika ndoa na tayari wamebarikiwa na watoto watatu pamoja. Pia wanalea mtoto mwingine mmoja, Morgan Bahati ambay Bahati alitoa kwenye chumba cha watoto.

Mwaka jana, Bahati alifunguka kuhusu mipango ya kufunga pingu za maisha na Diana Marua hivi karibuni.